NATURE AMTUPIA LAWAMA MB DOGGY KWA KUANZISHA MZIKI WA KUBANA PUA NA KUPOTEZA MZIKI WA KWELI

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

JUMA Nature amedai kuwa wasanii wengi wamemuiga, Mb Doggy na kusababisha muziki wa Bongo Fleva kupoteza mwelekeo kwa vile hawataki kufikiria kufanya kazi tofauti.

Nature amesema muziki wa zamani ulikuwa na mafanikio kwa kuwa wasanii walikuwa wakiimba kwa staili tofauti.

“Huko nyuma tulifanya muziki wenye ladha zinazotofautiana, kila mtu alijitahidi kufanya kazi yenye utofauti. Staili hii ya sasa maarufu ya kubana pua alikuja nayo Mb Doggy na kwa kweli nilifurahi kwani alikuwa amefanya kitu chenye utofauti,”  alisema.

“Lakini hali ni tofauti hakuna aliyekuja na wazo lingine, wote bado wapo palepale. Ni vyema tukajifunza ubunifu ili sanaa yetu isonge mbele.”

Alitoa ushauri kwa wasanii wa sasa kuwa wangeacha kuimba nyimbo za mapenzi na badala yake wageukie jamii ili kuweza kutoa elimu katika nyanja mbalimbali.

“Nikipanda jukwaani naimba nyimbo zangu za mwaka 2000 hadi 2012 lakini zote ni kama ndiyo kwanza nimezitoa, ni kwa namna mashabiki wanavyozipenda,” alisema Nature (pichani).

Alipoulizwa kuhusu hilo, Mb Doggy alisema: “Ubunifu wangu ulikuwa mzuri, namshukuru Mungu nilibuni kitu kinachoishi ila si kwamba nimeua Bongo Fleva. Kilichopo ni kwamba vijana wa sasa wapanue mawazo ili waje na kitu bora zaidi, ni kweli kuwa kila mtu sasa anaimba kama mwenzake.”
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

8 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Safi sana j nature

    ReplyDelete
  2. Asante san bro NATURE,umesema ukweli,ck hiz wasanii wanaimba mziki unaofanana

    ReplyDelete
  3. Sasa hivi hamna wasanii kuna wauza sula, mziki hauna athari kama wa zamani, wao umaambie kuvaa nguo za dada zao 2. PUUMBAAFUUU!!

    ReplyDelete
  4. Mchelemchele wamejaa siku hizi hakuna wasanii

    ReplyDelete
  5. Mi namkubali sana huyu Jank...na truck latest track yake imenibamba mbaya..Dogo aka Kaza!! Dah mwanangu style yako ya kuimba iko pouwa sana

    ReplyDelete
  6. Nature huna jipya shoga2 wew

    ReplyDelete
    Replies
    1. wewe unaemtukana nature chizi amekukosea nini

      Delete
  7. HUYO NATURE KASHAFULIA,HANA JIPYA NDO MAANA ANAANZA KUJIFANYA JUDGE WA WENZAKE! YEYE MIAKA YOTE NI KUVUTA BANGI,KULA KUBERI,KUNYWA GONGO N.K,STYLE YAKE TANGU MIAKA YA NYUMA NI ILEILE! LAZIMA AKUBALI MATOKEO KUWA SASA HIVI KUNA DAMU CHANGA ZINAPIGA SHOW ZA KUFA MTU,ZINA MAFANIKIO YA HATARI! ME NINGEKUWA YEYE,NINGEOMBA TU KUFANYA JAPO COLLABO NA HATA MSANII MMOJA AMBAYE YUPO KWENYE CHART ILI NIINGIZE MKWANJA.KUDISS SI SOLUTION!

    ReplyDelete

Top Post Ad