ZITTO AWAOMBA WAKAZI WA KIGOMA KUMUUNGA MKONO KWENYE VITA YAKE NDANI YA CHADEMA

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe amewaomba wakazi wa Mkoa wa Kigoma kumuunga mkono katika mapambano yake ndani ya chama hicho. 
Akizungumza Mjini Kasulu katika mkutano wa hadhara, Zitto alisema atahakikisha anapigania haki yake ndani ya Chadema kwa kufuata taratibu zote zilizowekwa kwa mujibu wa Katiba ya Chama hicho ili aweze kurudishiwa nyadhifa zake, hususan nafasi ya Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Bara aliyovuliwa na Kamati Kuu Novemba 21, 2013.

“Najua nakabiliwa na vita kubwa ndani ya Chadema, lakini kwangu mimi (Zitto) hii ni changamoto, naamini nitashinda tu. Lakini lolote litakalotokea ndani ya Chadema hata kama ni kunifukuza, nitarudi kwenu ndugu ili tuamue kwa pamoja nini tufanye, wapi twende kwa pamoja kama tulivyo kwani nguvu ya mamba ipo kwenye maji,” alisema Zitto.
Amesema kwa kipindi kirefu anaonekana kama msaliti ndani ya chama na anatuhumiwa kutoa siri za Chadema kwa CCM na Serikali. “Tuhuma hizi hazina ukweli, nalaumiwa na kubambikiwa mambo kutokana na msimamo wangu ndani na nje ya chama
“Watu wa Kigoma ambao ndiyo tulipokea mageuzi kabla ya wengine, tunaitwa wasaliti ndani ya Chadema, lakini waliokuja baadaye kutoka mikoa mingine hawa ndiyo wanajiona wasafi. Wapo Watu waliingia Chadema baada ya kukosa fursa za kugombea huko walipokuwa awali na sasa wanajifanya ndiyo Chadema damu-damu. Sitoki Chadema ng’o, labda wanifukuze,” alifafanua Zitto. “Mnakumbuka misukosuko iliyomkuta Dr Kabourou (Aman) alipokuwa Kiongozi wa Chadema, pia walimwondoa Kafulila (David) na sasa mimi (Zitto) natafutwa ili niondolewe. Lazima tuungane pamoja kutetea masilahi yetu watu wa Kigoma,” aliongeza Zitto.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

6 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. zito wapeleke hao hd demokrasia ya kweli ipatikane@ Zito We Ni Shujaa

    ReplyDelete
  2. Tapeli wa siasa, msaliti. China na Korea Kaskazini wasaliti wanapigwa kamba shingoni.

    ReplyDelete
  3. Watamuunga mkono mataahira wenzake...binafsi sina muda wa kuunga mkono upuuzi

    ReplyDelete
  4. huyu kijana angelitulia angefika mbali, tamaa zinampoza, hana lolote, ndiyo waumizaji wa maendeleo hawa, wanajali matumbo yao tu.

    ReplyDelete
  5. Zito wewe Ni Kamanda! HUYO muhuni anaejiita Kamanda Wa Anga hana Lolote na hawa Ni mademu wAke tunaowafahamu!!!grace Kiwelu!! Irene Lema!!! Chiku Agwao na Joyce mukya!!! Ndio Habari ya mutiny !!!!

    ReplyDelete
  6. acha ubwege wewe, sasa mademu hapa wanahusika vipi? nani aliyekwambia zito hana mademu? kwanza hata ndoa ajafunga, atuongelei kuhusu mademu hapa, hayo ni mambo binafsi ya mtu na hayakuhusu

    ReplyDelete

Top Post Ad