MTANDAO WA UNGA WA JACK PATRICK UNATISHA

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Na Mwandishi Wetu
BADO habari ya mjini ni skendo ya kunaswa na madawa ya kulevya ‘unga’ inayomtafuna Video Queen wa Bongo, Jacqueline Clifford Fitzpatrick ‘Jack Patrick’ ambaye inadaiwa kuwa mtandao wake wa biashara hiyo ni wa kutisha, Ijumaa limetonywa.

Habari kutoka kwa rafiki wa karibu wa Jack ambaye aliomba chondechonde asitajwe, alidai kwa sasa vigogo wanaojihusisha na biashara hiyo haramu wamekuwa wakihaha kwa hofu kuwa modo huyo anaweza kuwataja hivyo wanafanya kila linalowezekana ili wamnusuru kama ilivyokuwa kwa Agnes Gerald ‘Masogange’.

Ilisemekana kuwa katika mtandao huo, vigogo hao wenye maskani jijini Dar, Rwanda, Uganda, Kenya, Dubai, Thailand, Italia na Hong Kong wamekuwa wakihaha kumuokoa Jack bila mafanikio.
“Unajua China siyo rahisi kumchomoa kama ilivyokuwa kwa Masogange (Agness Gerald) aliyenaswa Sauz (Afrika Kusini) kwa sababu wale (China) Tanzania haikuwasaidia kupata uhuru kama ilivyokuwa kwa Sauz.

“Ile ngoma ni mbichi, hakuna upenyo wa rushwa pale. Ngojeni tusubiri hukumu maana itakuwa kali sana, nazijua vizuri sheria za China juu ya madawa ya kulevya,” alisema rafiki huyo wa Jack na kuongeza:

“Hakuna ishu iliyoniuma kama ya Jack kwa mwaka uliomalizika.”
Katika nusanusa za gazeti hili, ilidaiwa kuwa bosi aliyemtuma Jack ni mwanamke mmoja tajiri aishie jijini Dar ambaye ana mtandao mkubwa wa biashara hiyo duniani.

Ili kuthibitisha kuwa mtandao uliodaiwa kumtuma Jack unatisha na una watu wazito, ilielezwa kwamba mrembo huyo hakuwa peke yake kwani alifuatana na warembo wawili, mmoja Mtanzania na mwingine raia wa Rwanda ambao wao walifanikiwa kuwatoroka polisi wa China.

Mbali na timu hiyo ya watu watatu waliokuwa na mzigo mwilini, pia kulikuwa na mtu mwingine aliyekuwa akiwasindikiza.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

8 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. wamminye mpaka awataje, sababu hawakomi hawa wauza unga, wanatuharibia vijana wetu, shenzi kabisa.

    ReplyDelete
  2. Shetani ndiye mtawala wa dunia hii na muongozo maovu. Hivyo basi lazima mtandao huo uwe mkubwa sana.

    ReplyDelete
  3. Lkn kwa nini anyongwe peke yake inabidi China kama kwl inafata haki na usawa wawatafute na walio mpa uo mzigo waukumiwe wote kwa kufanya ivyo watakuwa wanapunguza uo mtandao kuliko kumuhukum mwenyewe, kwan hao vigogo watatuma watu wengine tene, na unajua watu wanashida wanawapata, lkn wakijuwa watu wao wakikamatwa na wao wanakuwa wameisha awawezi kufanya ivyo

    ReplyDelete
  4. MANGE KIMAMBI muulize mzigo wake aliubeba Vipi na akarudi shwaaari .Haya mambo muwaachie watoto wa mjini

    ReplyDelete
    Replies
    1. na wewe je elezea mzigo wako uliubebaje mbona hujakamatwa...na mtamuota sana mtoto wa watu mtaishia hivohivo kuweweseka kuma weee

      Delete
    2. Mbona una roho mbovu hivyo wewe? hata kama humpendi mtoto wa watu acha kuzusha mambo yasiyo na ukweli. Karma ipo hapa hapa duniani.

      Delete
  5. Each goat will eat according to the length of its rope ...life is everywhere its ol abt tryng

    ReplyDelete
  6. Nilishawai kuwa rafiki na Mhe mmoja kwa sasa Ni war mambo nyeti!!' skins akanimbia mambobo hayo ya sembe nilitimua vumbi mbaya!! Nikakumbuka kwetu kulivyo na mashamba ya kulima!! Eti nikamatwe na sembe ukoo wangu wangenishangaa sn!! Halafu Mungu angenipa pigo jamani!!!

    ReplyDelete

Top Post Ad