MWANAFUNZI IFM AKUTWA AMEFARIKI CHUMBANI, SOMA KILICHOTOKEA HAPA

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mwanafunzi wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Ibrahim Jackson (24), amekutwa akiwa amekufa katika chumba cha kupumzikia kilichopo chuoni hapo bila mwili wake kuwa najeraha lolote.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Marietha Minangi, alisema tukio hilo lilitokea saa 11:30 juzi jioni katika chumba namba 118 jengo namba D kilichopo mtaa wa Shaban Robert.
NIPASHE lilifika IFM na kuzungumza na Mshauri wa Wanafunzi, Emmanuel Mushi, ambaye alisema kuwa marehemu alikuwa anasomea Shahada ya Usimamizi wa Kodi akiwamwaka wa pili.
Alisema marehemu alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa kifafa kwa muda mrefu kabla hata hajajiunga na IFM.
Alisema juzi jioni marehemu aliomba funguo kwa ajili ya kwenda kupumzika katika chumba kinachotumiwa kulala nawanafunzi kutoka nje ya nchi pindi wanapofika chuoni hapo kwa ajili yamasomo.
“Nyaraka zake zinaonyesha marehemu alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa kifafa kwa muda mrefu, hata kabla hajajiunga na chuohiki, kwa hapa chuoni ugonjwa huo ulikuwa unamtokea mara kwa mara,” alisema Mushi.
Aliongeza kuwa mara baada ya kupewa funguo alikwenda kupumzika katika chumba hicho na baadaye alikutwa amefariki huku mwili wake ukiwa umelala kitandani.
Alisema baada ya tukio hilo walitoa taarifa katika kituo cha polisi napolisi walifika katika chumba hicho na kumpeleka Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa uchunguzi zaidi.
Mushi alisema wamewasiliana na wazazi wake waliopo wilaya ya Mbozi Mkoani Mbeya na taratibu za kuusafirisha mwili huo zitafanyika leo.
Mmoja wa marafiki wa karibu wa marehemu, Peter Alphonce, aliliambia NIPASHE kuwa alikuwa na marehemu siku moja kabla ya kifo chake wakicheza mpira na walimaliza kucheza vizuri na kuagana kuelekea hosteli.
“Nilikuwa naye jana (juzi) tukicheza mpira, hadi saa kumi tulipomaliza aliniaga na kuelekea katika MachavaHostel ndiko anakolala,” alisema Alphonce.
@NIPASHE.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

9 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Acheni kupotosha jamii na habari zenu za kukopi na kupaste bila uhakika wowote, hili tukio limetokea tangu mwaka jana na wewe una copy na paste leo ukidai ni habari mpya.

    ReplyDelete
  2. Waandishi WA Bongo wakati mwengine ovyo kweli hii habari Ni ya muda mrefu we unaifanya mpya..

    ReplyDelete
  3. Uyu jamaa punga xana kama umekosa ya kufanya shughuli zipo nyingi kuliko kuipotosha jamii

    ReplyDelete
  4. mi napendekeza kungekua na uwezekano watu wanaotupotezea mda kusoma yaliypita jela miezi 2

    ReplyDelete
  5. Kamamazenu nyny wenye kukopy hizi habari kama ss wengine hatupo hapo tz si tunajua habari ni ya jana au juzi matako yenu

    ReplyDelete
  6. Ufara huu habari ya tangu March 2013 wewe unaweka January 2014 muwe na uhakika siyo kukurupuka kucopy na kupaste mamae

    ReplyDelete
  7. Hawa watu wa viblog wananiudhi sana, yani wao ni kopi n paste, sasa hv utaiona kwenye blog nyngne

    ReplyDelete
  8. Natamani nikujue maana umeonesha upungufu mkubwa wa Akili.Kuwa timamu bwana na kablogu chako.Punga mkubwa wewe.Unatuhadaa.Pumbaf.Unakopy tu bila kuhariri.

    ReplyDelete
  9. nonsenser bloger.....hivi unamaanisha nini, hivi umeishia la ngapi wewe hatujapendezewa sie tunajua habari ya mwaka huu, hebu kuwa mdadisi acha habari za kukopi na kupest

    ReplyDelete

Top Post Ad