TUSIMLAUMU JACKIE CLIFF...TUMLAUMU ALIYE MFUNDISHA KUVUA SAMAKI

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Jackie Cliff… mrembo wa haja niliyeanza kumfahamu kwenye video ya She Got A Gwan ya Ngwair. Ni msichana aliyeenda hewani na Mungu kampelea haswaa. Ukikutana naye huwezi kumwangalia mara moja ukaridhika, lazima ugeukE kumwangalia tena.

Nilipata bahati ya kumhoji mwezi September mwaka jana kwenye fashion show ya Ally Rehmtullah iliyofanyika kwenye hoteli ya Serena, jijini Dar es Salaam na katika maongezi yetu kuhusu Ngwair na kazi yake kama mrembo wa video nikagundua kuwa, Jackie ni msichana mpiganaji asiyejali kitu.

Jackie The Boss Lady, ni msichana anayejulikana kwa kuishi maisha ya kifahari yakiwemo kuendesha magari ya gharama ambayo wengi yaliwapa maswali mengi, ni wapi anapata fedha hizo? Ni kweli fani ya urembo inalipa hivyo? Sijasahau pia kuwa aliyekuwa mume wake, ni miongoni mwa madon wa Dar na ambaye alifungwa kwa miaka kadhaa kwa shutuma zile zile za sembe.

Huenda fedha alizokuwa akizitumia na kuziumiza roho za watu wengi zilikuwa za mume wake ama tayari alikuwa ameshaanza kufanya biashara hiyo haramu na ya hatari kabisa duniani.

Ni ngumu kujua nani aliyemuingiza Jackie kwenye biashara hiyo lakini uhakika mkubwa ni kuwa aliingizwa na mtu wake wa karibu, mume ama mpenzi wake. Kwa lugha nyingine ni kwamba, nyuma ya wasichana wengi wanaofanya biashara hii, wapo wanaume, madon wenye nguvu, madaraka, connection na fedha nyingi ambao si rahisi kuwafahamu. Hata wale wanaofahamika, ni nguvu kuthibitisha tuhuma hizo kwakuwa si wao wanaosafiri.

Kwa mtu kama Ray C, ambaye kukamatwa kwa Jackie hakumshtui hata kidogo kutokana na jinsi anavyowachukia wafanya biashara wa sembe, naamini anapata hasira kufahamu ukweli huu kwamba, wasichana hawa wanatumiwa tu.

Kuna watu wakubwa nyuma yao. Matajiri wakubwa katika nchi hii ambao ukitaka kuwajua, unaweza kujikuta pabaya hasa kama unaishi kwenye nchi kama Tanzania ambayo fedha inaongea kuliko haki na rushwa imetawala. Ni rahisi kudeal na majambazi kuliko kudeal na wazee wa unga. Wale waliojaribu wanajua vitisho walivyovipata. Biashara ya unga ni hatari kwa vijana wengi wa Tanzania na wauzaji wanajua hilo, lakini kamwe hawawezi kukubali kuona unawaharibia ugali wao.

Akina Jackie, Agnes na wengine, ni mfano tu wa wasichana wengi warembo na mastaa wa Tanzania wanaotumiwa kwenye biashara hii haramu. Wapo wengi, wanaume na wanawake, wenye majina na wanaofanya kazi hii. Naamini siku moja atakuja kukamatwa mtu asiyetegemewa kabisa na kila mmoja atabaki mdomo wazi.

Pengine kinachowaponza wasichana wengi, ni kutaka kuishi maisha yasiyo yao. Hupenda kuishi maisha ya anasa na starehe. Kwa mji kama Dar es Salaam na maisha fake ya Instagram yanayooneshwa na wasichana wengi wa Kibongo, inahitaji moyo kwa msichana mrembo kuvumilia kuishi maisha ya kawaida.

Na ndio maana, wengi hujikuta kwenye himaya za wauza unga ambao pamoja na kuwageuza chombo cha starehe zao za kimwili, huwaingia kwenye biashara hizo hatari na hata kama uhusiano ukiisha, wengi hushindwa kujitoa.

Wakati ambapo kila mtu anamsema vibaya Jackie na kumkejeli kwa kila neno, tujikumbushe kuwa, nyuma yake wapo watu wazito na hatari zaidi. Jackie kafundishwa tu kuvua samaki na aliyemfundisha haoni shida kutafuta msichana mwingine wa kuziba pengo hilo na biashara itaendelea.

Kama ilivyo kwa Jackie na hata kwa Agnes Masongange, ukifanikiwa kuufuatilia mlolongo wa wahusika, ni lazima ukufikishe kwa mtu mzito anayewapa kazi hizo. Kwakuwa safari moja tu ya kupeleka ama kuleta madawa nchini na iliyofanikiwa inaweza kubadilisha maisha yao kabisa, wasichana wengi warembo wameshindwa kukataa ofa hizo.
Hujiulizi kwanini wanaotumiwa kwenye safari hizi karibu wote ni wasichana warembo?

Kwa muda mrefu, kumekuwepo uhusiano mkubwa kati ya urembo na biashara hiyo. Si Tanzania tu, bali ni duniani kote.
Hii ni kwasababu ni ngumu kuhisi ‘uharamu’ wowote kwenye sura nzuri ya msichana na tena anayejulikana kwa kazi nyingine tofauti. Kama ya ulimbwende.

Swali la kujiuliza, ni kwanini madon hawa huwatumia zaidi warembo wa video ama Mamiss? Hadi sasa watatu wanafahamika kunaswa na mtego. Binti Kiziwi ambaye amefungwa nchini China, Jackie Cliff ambaye naye kifungo kinamngojea na Agnes Masogange ambaye kesi yake iligeuka kuwa nyepesi na kuhukumiwa kulipa faini tu.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

11 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. inasikitisha sanaa, hili ni janga la Dunia nzima sio tanzania tu, kila lenye mwanzo halikosi kuwa na mwisho, hata hao wanaowatuma sidhan kama wanaishi kwa amani! mwisho wao utafika, malipo ni hapa hapa Dunian ukiua kwa upanga na wewe utauwawa kwa upanga!! Tafakari

    ReplyDelete
  2. eeh Mungu ni wewe tu ndo unaweza kuukumu hawa watu, wamalize, anza na hao madon sijui, mlaaaniwe, tumieni watoto wenu...

    ReplyDelete
  3. me nalia na madoni tu, serikali jamani yakamateni hayo, yanauwa watoto zenu, angalia huyu mrembo sasa, sijui wachina watamfanya nini?

    ReplyDelete
  4. So sad mungu atamsaidia

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mungu atamsaidia kwani ndiye aliyemtuma?acheni kumsingizia Mungu,alitumba akatupa akili na utashi pia.

      Delete
  5. ni bora wanyongwe hasa huko china! k#mamazao!



    ReplyDelete
  6. aisee hii sasa taabu. kumbe ana undugu na binti kiziwi na aliwahi kusema kuwa akienda china huwa anaenda kumtembelea gerezani. na siku binti kiziwi anakamatwa airport jack alikuwepo, sasa zamu yake ikafika....jack atakuwa alikuwa anawindwa na pepo la kutokuskia....yaani uone mwenzio kakamatwa mbele ya macho yako, na una ushahidi kuwa kweli yupo gerezani na bado hukomi unarudia same mistake????? mbaya zaidi ni hizo tetesi kuwa jack ndo alikuwa anambebesha binti kiziwi.....aisee hii mbaya.

    ReplyDelete
  7. Jacky kakosea , kavunja sheria kwa makusudi na nilazima aadhibiwe! Kazi kaifanya kwa muda wa miaka 5...kukamatwa haikuwa bahati mbaya ila ilikuwa mwisho wa uovu wake. I hope I kitoka atajifunza kuridhika na maisha alio pangiwa na Mungu...na sio kuuza sembe wala nyapu!

    ReplyDelete
  8. udaku acha izo,huyu akutumwa kuvua samaki,huyu alitumwa kwenda kuangamiza roho za wenzake,kwani alikuwa analala na njaa,alikuwa anatembea uchi kwa kukosa hela au alikuwa analala porini? Si alitamani kuishi kama rihanna?ya kaisali mpeni kaisali ayanye yake

    ReplyDelete
  9. Wadau happy new year!!! Nimerudi tar 1 kutoka London nawaambieni nimepata shida airport sn!! Kwenye ndege tulikuwa 3 waafrika!!MIMI mtanzania! Mnaigeria1 na mkenya MIMI niliingiingizwa chumba maalum kwenye Mashine maalum! Nikatoka Hapo nikaletewa mbwa mweupe akanizunguka!! Nikapelekwa kwenye computer!!!! Jamani ndege ilichelewa dk3 kwa ajili yangu MIMI mtz nini hii!!'

    ReplyDelete
  10. WAKAMATWE HAIJALSH N NAN,WANAFIKIR RIZ ONE ALVYOACHWA UKO CHNA NA WAO WATAACHWA,WAKINYONGWA NDO INAPENDZA ZAID COZ WAO WAMEUA SANA,

    ReplyDelete

Top Post Ad