BAADA YA DOGO JANJA KUOMBA MSAMAHA ILI ARUDI TIP TOP, HII NDIYO KAULI YA MADEE NA BABU TALE VIONGOZI WA TIP TOP

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Dogo Janja kuuomba msamaha kupitia vyombo vya habari uongozi wa Tip Top Connection na Madee aliyemtoa Arusha, Boss wa Tip Top Connection Babu Tale ameiambia tovuti ya Times Fm kuwa anataka rapper huyo aseme ukweli wa yote aliyoyasema awali baada ya kutoka Tip Top.

“Aongee ukweli tu haina shida, nimemsamehe yeye ni Muislamu mwenzangu tumetumwa tusameheane, mimi nimeshamsamehe ila nimezungukwa na mashabiki ambao wakati yeye ananitukana kuna mashabiki ambao walikuwa upande wangu ingawa walikuwa hawajui kama dogo alikuwa anaongea ukweli au uongo.” Amesema Babu Tale.

“Babu Tale ameweka wazi vipengele ambavyo anataka Dogo Janja aviweke sawa.

“Dogo anatakiwa aseme kama kweli aliibiwa, kama kweli alidhurumiwa na kama kweli hajawahi kuishi nyumbani kwa Madee. Anatakiwa aongee dhahiri asifiche, aongee tu ukweli.” Babu Tale ameeleza.

Amegusia pia tukio ambalo lilimsikitisha zaidi wakati Dogo Janja anafanya kazi akiwa chini ya menejimenti ya Mtanashati Entertainment.

“Siku zote kwenye ukweli uongo hujitenga, wakati yuko South Africa alipost picha ‘ningekuwa Tip Top nisingefika huku’. Nilishangaa heeh huyu kutoka huko kijijini kwao alifanyaje hadi kufika hapa!

“Wazazi wake nao wakawa wamekubali uongo wa mtoto wao wakaanza kutuongelea na sisi maneno ambayo ni uongo. Ulikuwa uongo wa watoto halafu bado wao wanakandamiza uongo zaidi ya uongo. Kwa kuwa ni mtoto kuna wazazi ambao walisimama nyuma yake ambao nao walikuwa wanasapoti. Aongee ukweli mimi ntamsaidia.” Babu Tale ameeleza.

Babu Tale ameeleza kuwa Dogo Janja ameshamtafuta kwa njia ya simu lakini amemwambia ujumbe ule ule kuwa awaambie ukweli watanzania.

Kwa upande wa dogo janja, ameongea na Tovuti ya Times Fm na hakutaka kuizungumzia kwa undani kauli ya Babu Tale, zaidi alieleza kuwa alichokifanya kuomba msamaha alimaanisha kuwa alikuwa amekosea na hakuna aliyemsukuma kufanya hivyo.

Ameeleza kuwa endapo atakaribishwa tena Tip Top Connection atajiunga na kundi hilo japo ameeleza kuwa kuomba kwake msamaha hakuwa na maana kuwa alikuwa na lengo la kurudi Tip Top.

“Mimi nimeomba msamaha kwa kuwa nataka kuweka mambo sawa na kumaliza tofauti na uongozi wangu wa zamani. Hivyo tu. Wakinikaribisha Tip Top itakuwa poa tu pia…fresh.”

Times Fm ilimtafuta Madee ambaye alisema kuwa bado hajawa tayari kuongelea suala hilo na kwamba mtu anaeweza kuzungumzia suala hilo kwa sasa ni Babu Tale.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

9 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Huyo babu tale ni mngese analeta mambo ya udini

    ReplyDelete
  2. tena unataka alete ya kishetani au

    ReplyDelete
  3. babu tale yupo right. Huyu dogo ndiye mwenye matatizo ,japo wengine wanaweza wakasema anaonewa, si kweli, mimi sio fan wa dogo wala babu tale, ila kwa wasiomjua dogo janja. utoto ndio tatizo lililomkuta. na babu tale ameonekana mbaya hata kwa wazazi wa dogo, ndio maana anataka mambo yawe wazi.kitu ambacho hata mimi ningekubaliana na wao. huu ni usanii huwezi kuwa juu siku zote dogo janja anatakiwa ajue hivyo.Tatizo dogo janja elimu nayo finyu sana na ukichanganya na utotowake, anahitaji kurekebishwa ili akue kimaadili.kwa umri wake si wa kumchapa fimbo kwani ni msanii na anaheshimika kwenye jamii kwa namna fulani.anatakiwa aelimishwe kama hivi.

    ReplyDelete
  4. Kiukweli.bila kuficha.dogo alishawah.kukataa kwamba avuti.bangi lakin watu wanazopicha anapasha.cha arusha...na ndivyo.walivyo hawa wasanii.wetu ndio unanyonya.basi ondoka.kama ulivyo.kuja usiwe na kashfa..mara unataka.kurudi.dar unachezea.dar.nn..huku ndo kila kitu..utakimbia hutarudi.tuu..big up tale na madee

    ReplyDelete
  5. Kiukweli.bila kuficha.dogo alishawah.kukataa kwamba avuti.bangi lakin watu wanazopicha anapasha.cha arusha...na ndivyo.walivyo hawa wasanii.wetu ndio unanyonya.basi ondoka.kama ulivyo.kuja usiwe na kashfa..mara unataka.kurudi.dar unachezea.dar.nn..huku ndo kila kitu..utakimbia hutarudi.tuu..big up tale na madee

    ReplyDelete
  6. huyo tale anajielewa.Ndo maana anatoa wasanii wazuri.

    ReplyDelete
  7. Huyo dogo si aweke wazi tu hayo mambo ambayo tale ameyasema kama kweli ameamua kuomba msamaha wa kweli

    ReplyDelete
  8. ukweli ni kwamba bila madee dogo acngetoka......kabla ulikua unamtegemea sana madee akutoe lkn ulivyotoka tu ukajiona bonge la mjanja,pole dogo!

    ReplyDelete
  9. Ni kweli hata mimi huyu dogo aliniudhi sana kwa maneno aliyokuwa akiyatoa katika vyombo vya habari kuwakashifu tip top hasa madee,Madee hakuwa na kosa nionanyo mimi kwa sababu alikuwa anajaribu kuplay part ya mzazi kwa kumuhimiza ktk masuala ya shule ambacho ni kitu kizuri tu kwa dogo kingeweza kumsaidia baadae katika maisha yake mwenyewe sasa yeye akaona ananyanyaswa,sasa anaombaje huo msamaha ilhali yeye ndio aliyekosewa?kwa mantiki hiyo basi mimi naungana na babu Tale moja kwa moja kwamba aieleze kinaga ubaga jamii kilichotokea afu mwisho wa siku namshauri na madee amsamehe tu dogo kwa kuwa alikuwa hajui alitendalo na huo ndio ubinadamu.

    ReplyDelete

Top Post Ad