JE, MH. SITTA AMECHUJA AU AMEPAUKA?

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Alipokuwa spika wa bunge la 9,alitupa mwamko wa kufuatilia vikao vya bunge.Hasa pale aliporuhusu uundwaji wa kamati ya Mwakyembe iliyochunguza dili la richmond na hatimaye kupelekea kumwagika kwa unga wa EL.Wengi tulijua kuwa mzee amedhamilia kuleta mapinduzi ya kisiasa,kwamba hajali ni mtu wa chama gani,ila anachojali ni viwango na kasi.

Juzi ameaminika na kuchaguliwa kwa kishindo pale bungeni ili kuongoza bunge la katiba,akarudia katika maelezo yake kuwa atakuwa yule yule wa viwango na kasi,wengi wakampigia vigelegele,hata mimi nilifurahi na kurukaruka nikijua jembe limerudi shambani.

Ghafla,akatuacha solemba,akatuduwaza na kutuacha na mshangao mkubwa.Hii ilikuwa ni wiki jana pale alipokubali kanuni zisivunjwe ila zipindishwe.Ilikua amkaribishe JK aanze kuzindua bunge kisha afuatiwe na Warioba.Yeye 6,akapiga tiktaka akiwa amevaa taulo,akamleta kwanza Warioba ! Hii haikuwa kwa bahati mbaya,ila ilikuwa planned kabsaa! Yakawa yaliyokuwa na wote tumeshuhudia na kuhudhunika.Hivi kanuni walizojitungia zitafuatwa kweli kama wa kwanza kuzivunja ni 6 na rais wa nchi!?

Wadukuzi wa siasa zetu wanasema 6 alipewa shinikizo na chama chake ili aruhusu kwanza mwenyemeza wao(mwenyekiti) atanguliwe na Mzee Warioba ili baadae mwenyekiti aje kujibu mapigo.Vipi kama angetangulia mwenyekiti na kisha Warioba angefuata,je,mwenyekiti angesomeka kwa ile hotuba yake kweli?

Kwanini 6 anaonekana kuwa refa anayebeba timu fulani waziwazi? Mmeona kwenye kamati za uongozi alivyoteua?

Je, 6 amechuja au amepauka ?
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

10 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kachuja hana lolote huyo mbwiga tu

    ReplyDelete
  2. Nilikua namsikiliza six akimwambia jk aseme nini ile siku alipokua akihutubia bungeni, basi baba rizimoko akawa anarudia yote, ila mimi ndipo nilipo jiuliza uwezo wa six kutenda haki? Niaminini six atalinda maslahi mpaka hili bunge litavunjika. Mark my words

    ReplyDelete
  3. Mama ameonesha uwezo na kiwango kuliko 6. Unajua 6 alilewa sifa. Uwezo wske umepungua sana. Anatakiwa kutulia kama Bi mkubwa.

    ReplyDelete
  4. Makinda angefaa sana au pius msekwa. Nampebda makinda anavyoongoza bunge viherehere wote anawawezea

    ReplyDelete
  5. JAMANI, KUNA ALIYE NICHEKESHA LEO SIJUI NAYEYE AMEKAT TAMAA NA KUPOTEZA IMANI NA BUNGE HILI MAALUMU LA KATIBA KWA YANAYO JIRI KILA JIONI KAMA WENGI WETU WATANZANIA? ETI BORA WALE ABIRIA WA NDEGE YA MALAYASIA ILYOTEA WANGEKUWA NI HAWA WAJUMBE WA BUNGE LA KATIBA,INGEKUWA VYEMA..............

    ReplyDelete
  6. JAMANI, KUNA ALIYE NICHEKESHA LEO SIJUI NAYEYE AMEKATA TAMAA NA KUPOTEZA IMANI KWA BUNGE HILI MAALUMU LA KATIBA KWA YANAYO JIRI KILA JIONI KAMA WENGI WETU WATANZANIA TUNAVYO KUNA VICHWA? ETI BORA WALE ABIRIA WA NDEGE YA MALAYASIA ILIYOPOTEA WANGEKUWA NI HAWA WAJUMBE WA BUNGE LA KATIBA,INGEKUWA VYEMA..............

    ReplyDelete
  7. Unafiki umetawala

    ReplyDelete
  8. Huyu mzee anazeeka vibaya

    ReplyDelete

Top Post Ad