4/02/2014

FAHAMU HISTORIA FUPI YA WASTARA SAJUKI TOKA ALIPO ANZA KUIGIZA MPAKA SASA

Wastara Sajuki si jina geni kwenye ulimwengu wa bongomovies. Ni mmoja wa wanadada wanofanya vizuri sana kwenye filamu nchini na wenye ushawishi mkubwa sana ndani ya tasnia hii. Ifuatayo ni historia fupi ya mwanadada huyu.

Early life
Wastara Juma Issa alizaliwa Septemba 27, mwaka 1983 huko mkoani Morogoro. Mwaka 1989 akajiunga na Shule ya Msingi Mvomelo ‘A’ na kufanikiwa kumaliza elimu yake ya msingi mwaka 1995. .Mwaka 1996 alijiunga na Sekondari ya Agricalture mkoani humo.

Career
Mwaka 1999 Wastara aliingia rasmi kwenye sanaa ya maigizo na filamu yake ya kwanza kucheza iliitwa Utaishia kunawa akiwa na gwiji wa vichekesho nchini King Majuto.Mwaka 2004 mpaka 2006 alianza kuonekana kwenye mchezo wa Miale uliokua unarushwa na kituo cha television cha ITV

Akutana na Jennifer Mgendi

Wastara hakudumu sana kwenye kundi hilo, alikutana na kina Jenifa Mgendi ambaye pia walifanikiwa kuigiza naye filamu iliyowashirikisha baadhi ya wasanii wa kitambo akiwamo Dino na wengineo.

Mwaka 2007, Wastara alifanya usahili kwenye filamu ya mdau Ande John iliyofahamika kama Pelemende, akafaulu na kuigiza kwenye filamu hiyo kisha zikafuata filamu nyingine kama Penina kabla ya kutimkia nchini Kongo kufanya biashara.Akutana na Sajuki

Aliporejea kutoka Kongo, Julai, 2007, Wastara aliitwa na mwigizaji Shija ambaye alimuomba aigize naye filamu baada ya kumuona kupitia kazi mbalimbali alizowahi kufanya hapo nyuma.

Huo ndiyo ulikuwa mwanzo wa Wastara kukutana na Sajuki ambaye sasa ni mumewe wa ndoa kwani Shija alikuwa akifanya kazi zake za uigizaji kwa kupata msaada mkubwa kutoka kwa Sajuki.

Wastara alicheza filamu kadhaa akiwa na Shija pamoja na Sajuki hadi baadaye walipokuja kugundua kuwa matatizo ya uhusiano yaliyowakuta (Sajuki na Wastara) yanafanana kwani kila mmoja wao alitendwa na mpenzi wake ndipo walianzisha uhusiano wa kimapenzi.

 “Eeeeh! Kazi na dawa, tuligundua kuwa matatizo yetu yanafanana. Taratibu tukaanza uhusiano ili kufarijiana,” anasema Wastara.

FILAMU WALIZOZALISHA

Wakiwa ndani ya umoja wao, Sajuki na Wastara, walifanikiwa kuporomosha filamu zaidi ya 20 ikiwemo Mboni yangu iliyopata umaharufu mkubwa

 APATA AJALI

Wakati harakati za ndoa zikiwa zimepamba moto, mwaka 2009 Wastara alipata ajali ya pikipiki iliyosababisha akatwe mguu.

Wakati huo tayari alikuwa ameshachumbiwa na Sajuki.

Juni mwaka huo huo,

wasanii hao waliopitia changamoto kadhaa za maisha, walifunga ndoa na kuanza rasmi maisha ya mume na mke.

Baada ya hapo, kupitia kampuni yao ya Wa-Jey waliendelea kuzalisha filamu kama Briefcase, The Killers, Seven Days na nyinginezo.

Tarehe 2 mwezi wa kwanza (1) mwaka 2013 Wastara alimpoteza mume wake kipenzi Juma Kilowoko (sajuki) jambo lillilosababisha kupumzika sanaa kwa muda na badae alilejea kwenye tasnia na kutoa filamu ya Shaymaa amabayo ilipata umaharufu mkubwa

Nampaka sasa anaendelea kufanya filamu nchini Tanzania
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:
Loading...

1 comment:

 1. Utajiri wa nguvu za ujihni na ndagu JE UNAMATATIZO, (KWANINI USUMBUKE) NAITWA DR, MDIRO piga 0746796662. KAMA UNAITAJI PESA ZA MAJINI AU NDAGU YA MALI AU UTAJIRI NDANI YA MASAA 72(SIKU TATU), NDOA, MIKOSI, MABALAA, JINI MAHABA NA SHIDA YA UZAZI. NIPIGIE 0746796662. KIKUBWA NI KUSIKILIZA NA KUFATA MASHARTI. ANGALIZO USITUME SMS PIGA NA UWE NA NIA.

  (kuhusu utajiri au pesa) KABLA YA KUPIGA SIMU ZINGATIA YAFUATAYO
  1. uwe una umri wa miaka 18+
  2. uwe tayari kupokea masharti yote
  3.uwe na uwezo wa kutunza siri
  4. uwe jasiri wa kupokea taarifa yoyote .

  ReplyDelete

Loading...

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger