MR BLUE: WEMA, NAJMA WALINIFILISI

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Na Gabriel Ng'osha

NYOTA wa Bongo Fleva, Herry Samir maarufu kama Mr. Blue amesema wasichana warembo, Wema Sepetu na Najma ambao aliwahi kutoka nao kimapenzi kwa nyakati tofauti miaka ya nyuma, walimfilisi kutokana na matumizi makubwa ya fedha alipotoka nao viwanja.

Akizungumza na paparazi wetu hivi karibuni, Mr. Blue, msanii aliyeanza kupata umaarufu akiwa bado kijana mdogo, alisema alilazimika kutumia fedha nyingi akiwa nao, kwani vinginevyo wangemuona hana pesa, kitu ambacho hakuwa tayari kuona kinatokea.

“Mademu wengi walikuwa wanapenda sana starehe, kila day (siku) wanataka twende kiwanja, ndiyo maana kama unakumbuka niliyumba kimuziki.

“Wanawake wengi niliotoka nao hawajulikani, ila kuna Wema na Najma, ilikuwa ukizama nao dukani lazima ufanye shopping (manunuzi) ya nguvu, kuanzia laki saba, nane na kuendelea ili wakuone unazo na mademu wengi wakisikia tu umepiga shoo, sms hazikauki kuomba uwatumie mawe (pesa),” alisema.

Kuhusu maisha yake ya sasa, Mr. Blue alisema yamebadilika sana, kwani hivi sasa ameoa mwanamke mwenye asili ya Kiarabu na amejaliwa kupata mtoto mmoja, hivyo ni baba wa familia ambaye pia anakaribia kumaliza mjengo wake siku si nyingi.

Hata hivyo alisema mkewe siyo maarufu, ana malengo na upendo kwani amekuwa akimuaga kila safari anayofanya na kwamba hata yeye anaporejea nyumbani, hupokelewa vizuri.

Mr. Blue ni mmoja kati ya wasanii wa muda mrefu ambao bado wanafanya muziki na wenye mashabiki wengi ndani na nje ya Bongo.
GPL

----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

6 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Huna lolote unatafuta kick tu.

    ReplyDelete
  2. Hakuna kurudi nyuma bro, piga kazi kwa kwenda mbele. Familia yako kwanza, mengine baadaye

    ReplyDelete
  3. kwani ulitumwa uwe na wema na najma ni ubisho wako kijana mdogo kutaka wanawake wenye majina imekula kwako.

    ReplyDelete
    Replies
    1. na wewe ndio unajifanya mmarekani hata upendezi, kwanza hujui nini maana ya nigga, mtanzania huwezi kutumia neno nigga sababu sio utamaduni wetu, sema wewe shobo tu unashobokea black america

      Delete
  4. Kaza jomba ,tafuta salary ckuiz wenzako hawalali wanatumia pesa pesa...!

    ReplyDelete
  5. chezea wema sepetu

    ReplyDelete

Top Post Ad