TUCTA WAPIGANIA PAYE ISHUKE KWA WAFANYAKAZI

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

  SHIRIKISHO la Vyama vya Wafanyakazi (Tucta), limeazimia kuendelea kupigania kushushwa kwa Kodi ya Mshahara (PAYE) kutoka asilimia 13 inayokatwa hivi sasa hadi asilimia tisa, ili mfanyakazi apate ahueni ya maisha.

Katibu Mkuu wa Tucta, Nicholas Mgaya, alisema hayo jana Dar es Salaam wakati akizungumzia maadhimisho ya Mei Mosi yatakayoambatana na wiki ya wafanyakazi itakayoanza rasmi leo.

Maadhimisho ya Mei Mosi yatafanyika nchini kesho kutwa ambapo kitaifa yatafanyikia jijini Dar es Salaam na mgeni rasmi atakuwa Rais Jakaya Kikwete.

Mgaya alisema mbali na kupunguzwa kwa kodi, Tucta inayo mambo mengine mawili inayopanga kupigania ili ujumbe ufike serikalini na kupatiwa suluhu.

Suala la pili alitaja kuwa ni kila mfanyakazi kupatiwa malipo mazuri awapo kazini, jambo alilosema wamekuwa wakiliomba mara kwa mara na hadi sasa halijakamilika.

“Kila mfanyakazi ni mstaafu mtarajiwa, hivyo ni vyema waajiri waandaliwe malipo mazuri, ili mfanyakazi atakapostaafu awe na kiwango cha maisha kitakachomsaidia katika maisha yake,” alisema Mgaya.

Pia wamejipanga kupigania mifuko ya pensheni, ilipe kiwango sawa cha kiinua mgongo tofauti na sasa ambapo baadhi ya mifuko inalipa kiwango kidogo na mingine inalipa kiwango kikubwa.

“Ifikie wakati sasa kusiwepo na utitiri wa mifuko, bali ivunjwe na kubaki miwili yaani wa binafsi na wa umma ambayo mengine yanabakia yakijitangaza tu,” alisema Mgaya.

Mgaya alilitaja jambo lingine kuwa ni fidia kwa wafanyakazi ambapo alishauri kuundwe kwa mfuko ambao utawezesha mfanyakazi atakayeumia kazini, kulipwa fidia ambayo itamsaidia.

Kuhusu mabadiliko ambayo yametokea tangu maadhimisho yaliyopita ya Mei Mosi, Mgaya alisema ni kupungua kwa kodi kutoka asilima 14 kwenda 13 ambayo alisisitiza kwamba wafanyakazi wanaomba sasa ifikie asilimia tisa.

Gazeti hili lilimtafuta Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudentia Kabaka na Naibu wake, Makongoro Mahanga, wazungumzie mpango huo wa Tucta, lakini simu zao ziliita bila majibu.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. inakera sana hivi mtu anapokea laki moja akatwe asilimia kumi na tatu atabaki na ngapi ikiwa wabunge mawaziri hawakatwi kodi hi ni halali jaman ebu msijali matumbo yenu muwe na huruma, hamtaki kupandisha mshahara basi mpunguze kodi, kuna makampuni kibao hayakatwi hata kodi this is embar u know

    ReplyDelete
  2. kwel PAYE inatuumiza sn. wanajipendelea wao n familia zao huku ss wafanyakaz 2naoongeza pato la nchi 2nataabika

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ndo mjue nn maana ya kupiga kura ktk chaguzi.support those who support you.

      Delete
  3. kwel PAYE inatuumiza sn. wanajipendelea wao n familia zao huku ss wafanyakaz 2naoongeza pato la nchi 2nataabika

    ReplyDelete
  4. kwel PAYE inatuumiza sn. wanajipendelea wao n familia zao huku ss wafanyakaz 2naoongeza pato la nchi 2nataabika

    ReplyDelete

Top Post Ad