Akodi Ngoma Kumfumania Mkewe Akitoa Penzi kwa Rafiki Yake..Mtaa Wafungwa

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mwanadada aliyetambulika kwa jina la Asha baada ya kufumaniwa akisindikizwa na ngoma.
Na Dustan Shekidele, Morogoro
AMA kweli dunia ina mambo na mambo yenyewe ndiyo haya! Katika hali ya kushangaza, mwanaume aliyefahamika kwa jina la Ramadhan Ally, mkazi wa Kata ya Mbuyuni Manispaa ya Morogoro amewashangaza wengi kufuatia uamuzi wake wa kukodi ngoma ya asili kwa lengo la kwenda kumfumania mkewe aliyejulikana kwa jina moja la Asha.

Tukio hilo lililofunga mtaa lilijiri asubuhi ya saa 3:14  Jumatatu iliyopita eneo maarufu kwa jina la Sultani baada ya mwanaume huyo kutonywa kuwa, mke wake alikuwa amelala kwa rafiki yake kipenzi, Abdallah Elias.

Baadhi ya wananchi waliobahatika kuwasili katika eneo la tukio walishuhudia mwenye mali akiwashushia kichapo kikali ‘wasaliti’ hao ambapo vurugu zikapamba moto.

Kufuatia hali hiyo, viongozi wa serikali ya mtaa huo waliamua kutoa taarifa kwa Kamanda Mkuu wa Ulinzi wa Jadi Kata ya Mbuyuni, Aidan Mtimbo ambaye alifika eneo la tukio na vijana wake na kuwasomba watuhumiwa hao msobemsobe huku wakisindikizwa na ngoma hiyo hadi Kituo cha Polisi Kata ya Mbuyuni.

Katika hali ya kushangza, nje ya kituo hicho cha polisi baadhi ya wananchi waliokuwa na hasira walishinikiza watuhumiwa watolewe nje wawafanyie kitumbaya huku baadhi yao wakikipopoa mawe kituo hicho kilichokuwa na askari mmoja aliyevaa nguo za kiraia.

Baada ya vurugu hizo, afande huyo alipiga simu kituo kikuu cha polisi kuomba msaada ambapo askari wa pikipiki walifika na kuwakodia teksi watuhumiwa hadi kituoni.

Mwandishi wetu alifanikiwa kuwahoji wahusika wote watatu ambapo mume wa mwanamke huyo ndiye aliyekuwa wa kwanza kuzungumza kama ifuatavyo:
“Huyu mwanamke ni malaya sana, kwanza  nimemtoa kwao Matombo (Morogoro) akiwa na watoto wawili na kila mmoja na baba yake.

“Mimi sikujali hilo, ukipenda bonga penda na ua lake. Miezi mitatu iliyopita aliniambia ana ujauzito wangu, taarifa hizo zilinifurahisha sana. Cha ajabu juzi akaniambia ametoa mimba yangu, nilipomuuliza kwa nini, akasema kwa ujeuri eti hayupo tayari kuzaa na mimi kwa sasa.

“Nilichukua uamuzi wa kumrudisha kwao, jana usiku napokea taarifa kuwa yuko nyumbani kwa rafiki yangu kipenzi, Abdallah Elias.

“Ndiyo asubuhi nikakodi ngoma na kwenda, niliwakuta wamelala kitandani.”
Kwa upande wake Elias alipotakiwa kuzungumzia tukio hilo, alisema: 
“Huyu mwanamke ni mbaya sana, ametuchanganya mimi na rafiki yangu Dullah, yeye kaja kwangu jana Jumapili akaniambia  amefukuzwa na mumewe hivyo anaomba alale kwangu kesho  yaani leo aende kwao Matombo kumbe alisharudishwa kwao toka juzi.”

Naye mwanamke huyo alipohojiwa na paparazi wetu alikuwa na haya ya kusema:
“Huyu mwanaume (Ramadhan) hajanioa, kila siku nikimwambia twende kwa wazazi wangu ananipiga danadana. Ni kweli nimetoa mimba yake, siko tayari kuzaa naye mtoto nje ya ndoa. Huyu Elias, yeye alionesha nia ya kunioa.”

Diwani wa Kata ya Mbuyuni, Samuel Msuya amethibitisha kutokea kwa fumanizi hilo kwenye mtaa wake lakini aliwatupia lawama polisi wa pikipiki kwa kupuuza uongozi wa juu wa kata hiyo ambao kwa kushirikiana na walinzi wa jadi walifanikiwa kuwalinda watuhumiwa wao na kufika salama kwenye kituo cha polisi.
GPL
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Duu!! Huyo mwanamke noma! Kwa kwel ni malaya,na ww Elias mbaya sn,km alikuja kwako kutaka msaada kwa nn ucmpigie rafk yako kumuuliza?

    ReplyDelete
  2. homa ya jj n nan30 May 2014 at 11:09

    makubwa

    ReplyDelete
  3. Uyo demu syo kbx af muongo point zke zote za kijinga yan

    ReplyDelete

Top Post Ad