Hali ya Jack Gerezani Macau Nchini China Siyo Nzuri

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

UNAWEZA kusema ni majanga juu ya majanga yanazidi kumkumba modo wa Bongo, Jacqueline Patrick ‘Jack’ baada ya wiki iliyopita kushindwa kupanda kortini kufuatia kutetereka kwa afya yake bila kufafanuliwa. Mbali na kuwa na afya tete, pia Jack anadaiwa kulalamikia haki za msingi za kibinadamu ambazo anazikosa mahabusu kwa kuishi maisha kama ya mtu aliye kifungoni.

Akizungumza juzi jijini Dar, mtu anayejitolea kumpa msaada na kumtembelea Jack mahabusu, Macau, China alikoshikiliwa, Matilda- alisema Jack anaumia kwa kupewa maisha kama tayari amehukumiwa, anaona bora hukumu yake ipite ajue moja. “Kiukweli Jack anaumwa, alishindwa hata kwenda mahamani, mbaya zaidi hata wakili wake naye hakutokea siku hiyo.

“Halafu kule mahabusu anafanyishwa kazi ngumu ambazo hastahili kama mahabusu na amesema hata watu wake wa karibu ambao anaamini kwa kipindi hiki wangekuwa wanampa faraja hawaoni, anatamani angekamatiwa Bongo labda kuna watu wanapenda kwenda kumtembelea kule Macau lakini hawana uwezo.

“Wabongo wengi ambao wako Macau kwa ajili ya sanaa ya sarakasi ndiyo kidogo wanakwenda kumtembelea siku mojamoja,” alisema Matilda.
Juni 20, mwaka huu, Mbongo Fleva anayedaiwa ni mtu wa karibu na Jack, Juma Khalid ‘Jux’ na kumuuliza kwa nini hajawahi kwenda kumtembelea ‘bebi’ wake mahabusu kama wanavyofanya Wabongo ambao wako Macau, akajibu: “Sipendi kusikia ishu yoyote inayomuhusu Jack kwani nina mambo mengi ya kuongelea na si ishu za Jack kila kukicha.

“Kwa kipindi hiki sitahitaji mtu aniulize ishu za Jack, zinanitibua sana na kama kuongelewa zimeshaongelewa hivyo sioni kipya.” Hii ni mara ya tatu kwa Jack kupanda mahakamani, mara ya kwanza ilikuwa Aprili 10, mwaka huu kosa likiwa kukutwa na madawa ya kulevya tumboni aina ya heroin kete 57 au kilo 1.1 yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 223. Mara ya pili ilikuwa Mei 23, mwaka huu
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

7 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. What goes around come around!huyu mwanamke alichomfanyia mme wake kipindi amekamatwa ni mambo ya aibu sana ngoja na yy machungu yampate dunia imemfundisha

    ReplyDelete
  2. Hii ni dunia, bado flora mbasha malipo yanamsubiri.

    ReplyDelete
  3. This comment has been removed by the author.

    ReplyDelete
  4. dawa hizo zilikuwa zinaenda kuwaharibia watu wengi sana maisha. Haki itendeke kama kweli alihusika basi adhabu kali kwa mjibu wa sheria ni haki yake ya msingi.
    Kuhusu kupiga mzigo km ameshahukumiwa hilo halina tatizo kwa vile anakula na kutumia umeme,maji magereza so anataka ale, alale, anywe na alindwe bure mahabusu, she should work to pay that!
    Binafsi na omba haki itendeke na ionekane kutendeka pia.

    ReplyDelete
  5. SASA AJAHUKUMIWA ANALALAMIKA,ETI KAZ HAZIMUHUSU,JE AKIHUKUMIWA SI ATATOA MKUNDU ILI ASAIDIWE

    ReplyDelete
  6. atakoma, alivyokuwa ajitamba bongo eti bosy lady alifikiri sifa kazi kwake

    ReplyDelete
  7. Hivi serikali inasaidiaga watu kama hawa, au watakachoamua kumfanya ndio hicho hicho

    ReplyDelete

Top Post Ad