Kifo cha George Tyson Kuna Kitu, Mtabiri Ausishwa kuwa ni Mchawi

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Tatizo! Huku macho ya waigizaji na wadau wake hayajakauka machozi kufuatia vifo vya ghafla vya mwongoza sinema, Adam Philip Kuambiana (38) na mwigizaji Sheila Leo Haule ‘Recho’ (26), tasnia imempoteza mwingine, mwigizaji, prodyuza na mwongozaji filamu mahiri, George Otieno ‘Tyson’ (41).
Kufuatia kifo hicho ambacho pia ni cha ghafla, wadau mbalimbali wa filamu, wakiwemo wasanii wenyewe wamesimamia mawazo yao kwamba lazima kuna kitu!

Tyson alifariki dunia Ijumaa usiku akiwa njiani kukumbizwa Hospitali ya Mkoa ya Rufaa Mkoa wa Morogoro kufuatia ajali mbaya ya gari iliyotokea maeneo ya Gairo, Morogoro.

Katika ajali hiyo, mbali na marehemu walikuwemo watu wengine watatu ambao ni dereva, MC Gladness Chiduo ‘Zipompa’ na mwingine aliyejulikana kwa jina moja la Nick ambao walijeruhiwa vibaya na kupatiwa matibabu ya haraka.

WALIKUWA WAKITOKEA WAPI?
Gari walilopata nalo ajali ni Toyota Noah ambalo liliharibika mno. Wote walikuwa wakitokea Dodoma ambako Ijumaa mchana walirekodi kipindi na pia kutoa misaada ya madawati 60 kwenye Shule ya Msingi ya Chalula iliyopo Chamwino kupitia Kipindi cha Mboni Show kinachoongozwa na Mboni Masimba kupitia Runinga ya EATV.

Mboni yeye kama bosi wa msafara huo alikuwa kwenye gari jingine na watu kadhaa.

KISA CHA AJALI
Kwa mujibu wa chanzo, ajali hiyo ilitokea baada ya tairi la nyuma la kulia kupasuka ghafla kisha kufuatiwa na la mbele kushoto hali iliyosababisha gari hilo kupinduka na kubiringita mara tatu.

“Kwanza ilipobiringita mara moja, Tyson alichomoka kwenye gari, likabiringita tena mara mbili. Marehemu alipasuka sehemu ya kati ya paji la uso,” kilisema chanzo na kuanza kulia.
MANENO YA MWISHO YA MAREHEMU
Chanzo kilizidi kusema kuwa wakati marehemu anazingirwa na roho wa mauti alikuwa akisema ‘najua nakufa lakini nasikitika kuwaacha wanangu.’

KUNA KITU
Kwa upande wa wasanii kutoka tasnia ya filamu Bongo waliozungumza na gazeti hili juzi, walikazia dhana ya kuwepo kwa kitu kinachoondoa uhai wa wasanii kwa njia ya kufumba na kufumbua.

“Haiwezekani kila kukicha sisi tu. Tena ghafla. Aisee lazima kuna kiti japokuwa hatujakijua ni kitu gani,” alisema msanii na kiongozi wa Kundi la Jakaya Theatre, David Mponji ‘Lazi’.

Akaongeza: “Lakini nataka kukwambia kwamba huu ni mpango wa Mungu kabisa ili tufanye ibada. Unajua asilimia themanini ya wasanii hawaendagi kanisani wala misikitini? Hapa sasa tunakumbushwa.”

JACOB STEVEN ‘JB’:
“Hii ni too much! Kweli kifo sasa hata mimi nakiona kiko karibu. Nadhani kuna kitu.”

WILLIAM MTITU:
“Da! Sijui mimi niseme nini. Nadhani iko sababu ya kujiangalia, inakuwa kama kuna kitu vile.”

JACQUELINE WOLPER:
“Siamini aisee! Yaani juzi tu Kuambiana, akaja Recho, leo Tyson! Mh! Pana kitu hapa. Afadhali tungekuwa tumelia mpaka tumekauka machozi.”

WACHUNGAJI, SHEHE WAMSHUKIA MTABIRI
“Ukisema tabiri maana yake umba jambo. Ndiyo maana hata kwenye maandiko Mungu alimwambia nabii mmoja atabiri mafuvu kuwa binadamu, ikawa hivyo.

“Sasa huyu mtabiri (hakumtaja jina) ambaye amekuwa akisema wasanii watakufa kwa wingi ndiye ‘mchawi’ wao maana anaumba vifo kwa wasanii,” alisema Mchungaji Daniel Rashid wa Kanisa la EAGT Tegeta jijini Dar.

Baadhi ya wachungaji waliozungumza na Ijumaa Wikienda nao walionesha msimamo huo kwamba kutabiri ni kuumba.

Naye shehe aliyejitambulisha kwa jina la Hussein alipozungumza na gazeti hili juzi alisema yeye anaamini mtabiri ambaye amekuwa akisema wasanii watakufa ndiye mchawi wao.
“Kwanza kwa nini uwatabirie wenzako tu? Kuna nini hapo? Mbona sijawahi kusikia amejitabiria mwenyewe?” alihoji Shehe Hussein ambaye hakupenda kuuanika msikiti anaofanyia utumishi wake.

WOSIA MZITO KWA MASTAA
Katika hatua hiyo, viongozi hao wa dini walitoa wosia kwa mastaa wakisema kwamba katika hali kama hii hakuna njia mbadala zaidi ya kufanya ibada.
Walisema huenda pia vifo hivyo ni mpango wa Mungu ili kuwakumbusha kufanya ibada kwani wasanii wanaonekana muda mwingi wapo kazini kuliko kwenye nyumba za Mungu au hata kumkumbuka kwa maombi tu.

BONGO MUVI: HAKUNA KUREKODI FILAMU
Baadhi ya wasanii wa Bongo Movies waliozungumza na gazeti hili juzi walisema wanasikitishwa na vifo hivyo kwani kwa sasa imefikia hatua kwamba wanakosa muda wa kurekodi filamu, muda mwingi wapo kwenye misiba.

“Hatumkufuru Mungu kwani yeye ndiye muumba ila kusema kweli muda mwingi tunautumia kuzika tu. Filamu za kurekodi zote zimesimama, maana da!” alisema msanii mmoja akiomba hifadhi ya jina.

MWILI WA TYSON
Mwili wa Tyson ulitarajiwa kufikishwa Dar Jumamosi iliyopita kutoka Morogoro. Mjadala uliendelea hadi jioni ya juzi kwamba mwili wa marehemu ukazikiwe wapi kwa vile marehemu ni mwenyeji wa Kenya.

WAZAZI WAKE WAFICHWA
Habari za baadaye zilidai kwamba, hadi juzi jioni taarifa za kifo cha Tyson zilikuwa zimefichwa kwa wazazi wake kutokana na kile kilichodaiwa kwamba, hali zao kiafya ni ‘tiamajitiamaji’.

ASILI YA TYSON
Tyson alitua nchini mwanzoni mwa mwaka 2,000 akitokea Kenya. Alipofika alifanya kazi katika Kituo cha Runinga cha ITV akiwa ni prodyuza wa Kipindi cha Mambo Hayo.


Hapo ndipo alipomwibua Yvone-Chery Ngatwika ‘Monalisa’ na kumwingiza kwenye sanaa na baadaye kuwa mchumba wake ambapo mwaka 2001 walifunga ndoa ya kanisani.

Baadaye marehemu alijitoa ITV na kufanya kazi binafsi huku akiwa mwongoza sinema mahiri Bongo. Amekuwa mwongozaji wa vipindi mbalimbali kama Mboni Show cha Mboni Masimba, Wanawake Live cha Joyce Kiria na vipindi kibao vya TV1.

Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi Amina
GPL


----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. hta mi mwenyewe nliwaza yule mtabir c alitabiri haya mwaka huu wasanii watakufa wengi atakuwa ndo yeye anawamaliza mchawi anasingizia utabiri

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mdau tutajie jina. wengine hatukumsikia huyo mtabiri

      Delete
    2. anaitwa hussein ni mtoto wa shehe yahya aliyemrithi utabir!!!i

      Delete
  2. huyo mtabiri inabidi atafutwe apewe kichapo kuma mae zake

    ReplyDelete
  3. huyo mtabiri inabidi atafutwe achapwe kuma mae zake

    ReplyDelete

Top Post Ad