Serikali yamtuhumu Balozi wa Uingereza

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

 Serikali imetangaza rasmi mgogoro wa kidiplomasia kati yake na Balozi wa Uingereza nchini ikimtaka kujieleza kwa madai ya kuingilia mambo ya ndani ya nchi.

Mgogoro huo ulitangazwa bungeni mjini Dodoma jana na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Steven Maselle aliyemtaka balozi huyo kufika Wizara ya Mambo ya Nje kujibu tuhuma hizo.

Kiini cha Serikali kumtuhumu balozi huyo ni hatua ya Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila (NCCR-Mageuzi) kuihusisha Uingereza na urejeshwaji wa Sh76 bilioni za chenji ya Rada.

“Katika mchango wake (Kafulila), ameongea jambo moja nyeti sana na hili bora niliseme ili liwe fundisho kwa wengine… Hii ni nchi huru baada ya mwaka 1961,” alisema Naibu Waziri.

“Zimekuwapo ripoti kwamba Balozi wa Uingereza amekuwa akijihusisha kuratibu vikao mbalimbali katika Jiji la Dar es Salaam na Dodoma kinyume cha utaratibu na hadhi ya kidiplomasia.”

Huku akionyesha kuwa na hasira, Maselle aliongeza kusema: “Vikao hivyo vina malengo ya kuhujumu mipango na mikakati ya maendeleo, ushahidi huo upo na utakapohitajika utatolewa.”

“Inasikitisha na kuchukiza balozi wa taifa kama Uingereza akifanya vitendo kinyume cha maadili… Anahusishwa kushawishi marafiki wa maendeleo wasitishe misaada ya kibajeti kwa Tanzania,”alisema.

Balozi wa Uingereza

Hata hivyo, Mwananchi ilimtafuta Balozi wa Uingereza Dianna Melrose, azungumzie suala hilo, msemaji wake Tamsin Clayton ambaye ni Mkuu wa Kitengo cha Siasa, Miradi na Mahusiano alisema wameshtushwa na taarifa hizo, lakini kwa sasa hawawezi kusema chochote mpaka wafahamu chanzo cha tatizo.

Aidha Naibu waziri Maselle alisema kuwa hivi karibuni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), alikuja Tanzania na kwamba upo ushahidi kuwa Balozi huyo wa Uingereza, alitamka kuwa anafikiria kuishawishi Serikali yake isitoe fedha za Miradi ya Maendeleo ya Millenia (MCC2).

“Ni aibu kwa Serikali ya Waziri Mkuu, David Cameron kwa balozi wake kufanya uwakala wa Benki ya Standard Chartered, kuishawishi Serikali ya Tanzania ikope fedha ili kulipa kampuni binafsi,” alisema Maselle huku akipigiwa makofi na wabunge wengi wa CCM na kuongeza:

“Rais Kikwete amelikataa kwa nguvu zote…, Serikali haiwezi kubeba mzigo wa kampuni binafsi.”
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

8 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Afuate kazi yake na kilicho mleta nasio kuingilia yasiyo mhusu kibibi kizima kinafanya usenge wake big up massele na jk.

    ReplyDelete
  2. Please be sure to use correct images for your story. This is not a picture of Diana Melrose but of another official not even from the British High Commission. Don't get your stupid blog into trouble, remove the picture asap!

    ReplyDelete
    Replies
    1. Afu we mbuzi peleka vitisho uingereza nyokoooolo eti asap! Sa ndio utafanya nini

      Delete
  3. yes wazungu ndivyo walivyo unajua kwa sababu tz wana deal sana na wachina kibiashara, hivyo wanavuruga . ni kama issue ya Ukraine aliyeanzisha alikuwa ni kiongozi mmoja wa usa na shirika la ng,o kuweni makini na hizo ng,o zinazotoa misaada ndani yake kuna upenyezaji wa shughuli zao. ila wengi wetu hatujui nini kinaendelea.kwanza wote ni wanusaji.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Wewe haujui ukisemacho ndugu,mabalozi wa nje wapo kikazi zaidi, hawapo hapa kupiga siasa za ndio mzee kama mabalozi feki wa tanzania kina Chiligati,Adadi,Masilingi,Kamala nk nk.

      Delete
  4. Hao mafisadi hawapendi kuambiwa ukweli!ndio maana balozi mwingine wa uswis alipowaamnia kuna mabilioni yenu mwende mkachukue walisema amewadharau!hawa viongozi sio wakuoneea huruma hata kidogo ni mafisadi wakubwa.

    ReplyDelete
  5. wewe naibu waziri wa wishati na madini, steven maselle huo uhuru wa nchi yenu uko wapi, kama huru mbona mlikubali mfumo wa vyama vingi hali mlikuwa hamtaki.. usijidanganye na uhuru wa bendera hao ndiyo wanaowaongoza mtake msitake...... chezea british wewe

    ReplyDelete

Top Post Ad