Tapeli Lililojidai Kishoka wa Tanesco Ladakwa Live Mlimani City

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

TAPELI lililokubuhu kwa masuala ya kulaghai watu kwa njia ya kujifanya kishoka washirika la Umeme Nchini, Tanesco, jana asubuhi limedakwa baada ya kuwekewa mtego walipokuwa wakitaka kutapeli kwa mmoja wa Afisa wa Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) Bi. Usia Nkhoma- Ledama.

Kwa mujibu wa Bi. Usia akieleza tukio hilo, alidai kuwa  tapeli huyo alifika asubuhi  akiwa na wenzake sita,  nyumbani kwake  wakasema wanatoka Tanesco wamekuja kucheki mita ya Luku. Hata hivyo  wakakorokocha wakasema mita imechezewa kwa hiyo wanakata Umeme na kung’oa mita, eti waliona kwenye GPS  yao kuwaUmeme hauendi vema.

“wakasema fidia na kurudisha umeme kiofisi ni milioni 8! ila tukiwapa milioni 2 wataturudishia. nikawauliza kama mita imechezewa mbona tunanunua umemewa laki 3 kwamwezi? si ingepaswa tulipe kidogo? wakasema wakati mwingine wakiweka hiyo resistance (eti ndo kifaa cha kuiba Umeme) huwa kinafyatuka halafu  Umeme unakwenda zaidi! “ alielezea Bi. Usia.

Na kuongeza kuwa  vishoka hao wakakata Umeme wakaondoka, tujipange. tujadiliana na mzee tukapata mashaka maana walikuwa wakali halafu wanalazimisha mambo, wamevaa vitambulisho lakini wamevigeuza kwahiyo havisomeki. tukapiga simu Tanesco kuwauliza wakasema hao ni vishoka tuite Polisi,  basi tukawapigia simu waje wachukue laki tano waturudishie Umeme, mengine Jumatatu. wakaja fasta wakarudisha Umeme,  nikawaambia naenda aTM wasubiri nikawaacha na mzee nikatoka mbio mpaka Polisi chuo nikawahadithia wakanipa Polisi 3 nikaja nao nyumbani, tukawakuta wameondoka.

Mzee akawapigia simu waje hela imepatikana wakasema tukutane Mlimani City, tukafanikiwa kukamata mmoja wengine wakakimbia. tumemuacha selo, tukaandikisha maelezo. tunasubiri hatua itakayofuata.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad