UKATILI! Sangoma Amfyeka Nyeti Mtoto wa Mwaka Mmoja na kuingia nayo Mitini

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Ni jambo lililowaacha midomo wazi madaktari na wauguzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), jijini Dar es Salaam ambapo mtoto Almasi mwenye umri wa mwaka mmoja na miezi kumi (pichani akiwa na muuguzi) kufikishwa hospitalini hapo akiwa amekatwa nyeti na mtu aliyedaiwa ni mganga wa kienyeji ‘sangoma’ na kuipeleka kusikojulikana.

Akizungumza na Uwazi kwa masikitiko makubwa mwishoni mwa wiki iliyopita, baba wa mtoto huyo, Ismail Kamaga alisema tukio hilo lilitokea hivi karibuni katika Kijiji cha Omukagando, Wilaya ya Karagwe mkoani Kagera.

Alisema sangoma huyo aliyemtaja kwa jina moja la Adinali alifanya kitendo hicho  kwa watoto wawili akidai anawafanyia tohara.“Alidai anawafanyia tohara watoto wawili, baada ya muda mwenzake alipona wa kwangu hakuna kitu na nyeti aliondoka nayo, sina namna tena  ya kumsaidia mwanagu.

Nilimpeleka Hospitali ya Mugawa, Kagera ambako aliwekewa mpira wa kutolea haja ndogo na madaktari wakasema hawana jinsi.

Pia nilikwenda Kituo cha Polisi  Karagwe kuomba msaada wa kumkamata  mtuhumiwa lakini imeshindikana,” alisema baba huyo.

Mzazi huyo aliiomba serikali kumtafuta  mtuhumiwa akisema tukio alilolifanya ni sawa na kuuondoa uhai wa mtu.Kwa upande  wake,  muuguzi  wa  zamu aliyekuwa hospitalini hapo, Kulwa Kaombwe alisema kitendo kilichofanywa na mtu huyo si cha kuvumiliwa akaiomba serikali kuchukuwa hatua ili mtuhumiwa afikishwe kwenye vyombo vya sheria.

Kwa ujumla huyu mtoto amebadilishiwa  staili ya maisha na hicho ni kilema. Kumkata uume maana yake mtoto huyo hatapata mke wala watoto katika maisha yake,” alisema muuguzi huyo.

Kuhusu matibabu, alisema wanaendelea naye lakini tabu anayoipata Almasi ni kujisaidia kwa shida hasa haja kubwa.

Chanzo: Gazeti  la  Uwazi/Gpl
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad