Imebainika Ni Kweli Majina ya Waliofaulu Ule Usaili wa Uhamiaji Yalichakachuliwa

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Week Kama tatu zilizopita Udaku Special tuliweka Habari kuhusu Majina ya Waliofauli Usaili wa Nafasi ya Ukonstebo na Koplo Pale Uhamiaji ambayo ilisemekana yalikuwa yamechakachuliwa kwani wengi waliopata kazi hiyo walikuwa na undugu na wafanyakazi wa Idara hiyo, Baada ya Habari hiyo Serekali ilisimamisha mchakato huo kupisha uchunguzi , Leo taarifa zimepatikana kuwa ni ukweli majibu ya usaili huo yalichakachuliwa na kuwaacha waliofaulu na wahusika kuweka ndugu ama jamaa zao hivyo basi matokeo ya usaili huo yamefutwa rasmi Mpaka hapo Utakapofanyika Usaili Mwingine 

Akizungumza Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Mbarak Abdulwakil alisema hatua hiyo imechukuliwa baada ya kamati maalumu ya kuchunguza ajira hizo kubaini wazi kwamba waliopewa nafasi hizo hawakukidhi vigezo.

Abdulwakil alisema wizara imesikitishwa na udhaifu huo baada ya kubainika wazi kwamba malalamiko yaliyotolewa na wananchi na kusababisha wizara kuingilia kati na kufuta usaili wa kuitwa kwenye ajira kwa watu 200 ulikuwa sahihi.


Alisema baada ya kubainika kwamba kweli kulikuwa na upendeleo wa dhahiri kwani watahiniwa wenye sifa na waliopata alama za juu wakati wa usaili hawakuitwa na kukiukwa kwa vigezo vya wazi, ajira hizo zitatangazwa upya na kusimamiwa moja kwa moja na wizara na siyo idara hiyo kama ilivyokuwa awali.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. fanyeni hivi na BOT

    ReplyDelete
  2. ngojea nijaribu manake hata za TAKUKURU nazo zilikuwa hivyo hivyo full kujuana

    ReplyDelete
  3. hii ni kwa taasisi zote za serikali maana wote ni mchezo huo huo.

    ReplyDelete

Top Post Ad