Mwanaume Akishakupata Baada ya Muda Mfupi Upendo Wote wa Awali Huisha

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Hiyo ni kauli kutoka kwa baadhi ya wanawake.

Je kauli hiyo ina ukweli kiasi gani?

Kuna bahati mbaya moja, ambayo baadhi ya wanawake hawaijui. Hii ni ile yakudhani kwamba, mwanaume akishaanzisha uhusiano na mwanamke au wakioana, kiwango cha kupendana kitakuwa ni kile kile milele. 

Lakini ukweli ambao hawaujui ni kwamba, binadamu ana hisia na hisia hizi huweza kuchoka. watu wanapokaa pamoja au wanapokuwa pamoja katika uhusiano kwa muda mrefu, hufikia mahali ambapo kiwango cha hisia za upendo hushuka kwa maana kwamba, zimechoka.

Hebu fikiria inakuwaje ndugu au jamaa yako ambaye umekuwa ukitamani aje kukutembelea kutoka mbali anapokaa kwa muda fulani kwako, zile cheche za hamu zinapungua, wala bila kukosana au tatizo lolote? 

Ni hisia zimechoka, hata unaponunua nguo au kiatu kizuri sana, baada ya kuda fulani, ule 'mchecheto' wa awali kukihusu,hupungua au kwisha. Ni suala la hisia pia, si kwamba, hiyo nguo au kiatu hukipendi tena. Kama mwanamke halijui jambo hili, linapotokea, hudhani kwamba, mwenzake sasa hampendi, na ndipo hapo kauli kama:

''Mwanaume akishakupata baada ya muda mfupi upendo wote wa awali huisha''

Haya ni malalamiko ya wanawake katika kujaribu kuonyesha ushahidi wa hali hii. wanashindwa kujua kwamba, kabla ya kuanzisha uhusiano au kuoana, hisia zilikuwa bado ziko juu, kwa sababu bado watu hawa walikuwa hawajaanza kuwa pamoja kwa muda mwingi

Ni mwongo anayeweza kusema kwamba, katika mahusiano yake au ndoa yake hajawahi kuhisi hisia za upendo kwa mwenzake kushuka angalau kidogo. kuna kutofautiana tu katika viwango vya kushuka kwa hisia hizo. lakini kila binadamu hisia zake za upendo hushuka.

Kuna sababu nyingi zenye kufanya kiwango cha hisia za upendo kushuka lakini kubwa huenda ni maumbile, sababu nyingine ni uwezo wa kila mmoja kubadilika kufuatana na mazingira, uwezo wa kutenda na kutoa kauli nzuri kwa mpenzi wake katika mahusino. lakini pia utayari kwa kila mmoja kuondoa zile tabia ambazo mwenzake anasema zinamkera.

Kushuka kwa hisia za upendo hakuna maana ya kuondoka kwa upendo. Upendo unapoondoka umeondoka, lakini hisia za upendo zinaposhuka zinaweza kurudishwa na hali ikarejea kama zamani tu. wakati mwingine hurudi zenyewe kama zilivyopotea.

Lakini wapo baadhi ya wanawake hisia za upendo za wenzi wao zinapopotea,hubabaika na kuharibu mambo
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

12 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Basi kwa kuelewa hilo turuhusiwe tuwe na plan B haswa sisi wanawake... manake hisia zikipungua kwa mume unahamishia kwa kidumu

    ReplyDelete
  2. Nimekwelewa vizur mnoooo...

    ReplyDelete
  3. Nimekwelewa vizur mnoooo...

    ReplyDelete
  4. kwani hamnaga hizo plani B? mbona nyie ndiyo waaataalam wamichepuko?

    ReplyDelete
  5. siyo wanaume tu hata wanawake pia hisia hupungua muhimu wote wawili kujituma kuboresha penzi lenu

    ReplyDelete
  6. Mimi hisia hupotea kama mume akiishiwa!

    ReplyDelete
  7. alah..! kwa hiyo mwanamke ndio anatakiwa kupendwa tu.. duh. okeeee

    ReplyDelete
    Replies
    1. ndivyo vitabu vitakatifu vinavyosema

      Delete
  8. ILIVYO WANAUME HUWA WANATAMANI SIO KUPENDA . WANAWAKE WANATAKIWA KUELEWA ILA WANAWAKE HUWA WANACHELEWA KUPENDA PALE TU ANAPOPENDA NA KUTOA TUNDA BASI MWANAUME TAMAA INAKUA NDO IMEISHA KWA KUWA AMEPATA ANACHOKITAKA ANASEPA ZAKE NANDO MAANA WANAWAKE HUWA WANAUMIA SANA WANAPOACHWA KWANI TAYARI ANAKUWA KESHAMPENDA TOKA MOYONI. LAKINI MWENZAKE ALIKUWA KAMTAMANI TU.

    ReplyDelete
  9. kwa kawaida wanawake wanatakiwa kupendwa (Biblia imeagiza) na kupenda kuna maana pana upendo mkuu na usioisha huwa hauna kisababisho, hivyo wanaume wanatakiwa kudumisha upendo bila kuchoka wake zao hii ni pamoja na kutogeuza macho kama traffic police (kugeukia michepuko).

    ReplyDelete

Top Post Ad