Nyani Aliyejipiga Picha Azua Mgogoro

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mtandao wa Wikipidia umekataa kufuta picha ambayo Nyani ilijipiga ikisema kuwa kwa sababu picha hiyo ilipigwa na Nyani ambaye ni mnyama wala sio binadamu, basi inakuwa mali ya umma.
Hii ni baada ya mpiga picha, mmiliki wa kamera iliyotumika na Nyani huyo kujipiga picha, kusihi Wikipedia kufuta picha hiyo na kudai kuwa Wikipedia ilikuwa inaingilia haki zake za umiliki wa picha hiyo.
Mpiga picha, David Slater, alikuwa akijaribu kunasa picha za Nyani kwa masaa kadhaa, wakati ambapo Nyani mmoja alichukua mojawapo ya kamera za David na kujipiga mamia ya picha.
Picha hiyo aliyojipiga Nyani bila shaka ni ya kusisimua na imempeleka David kuwa maarufu ulimwengu mzima.
La kusikitisha ni kuwa hatimaye Slater sasa amejipata katika mvutano wa kisheria na Wikimedia kuhusiana na ni nani hasa mmiliki wa picha hiyo.
David, ambaye hutegemea upiga picha kama jinsi moja ya kujikimu kimaisha, yuko makini kuhakikisha picha hiyo imeondolewa kwa tovuti ya Wikipedia mara moja, huku Wikipedia ikidai kuwa iwapo kuna mmliki wa picha hiyo basi ni Nyani aliyejipiga picha hiyo.
Mvutano wa kisheria ilirejelewa kuangaziwa kufuatia uamuzi wa Wikipedia kuchapisha maombi yote iliyopata kuhusu kufuta au kuhariri habari au picha au video zozote ilizoweka kwenye tovuti zao.
Mojawapo ya maombi hayo ni David Slater kutaka picha aliyojipiga Nyani kuondolewa kwenye tovuti ya Wikipedia mara moja kwani ikiwa kwenye tovuti hiyo iko wazi kwa umma.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Duh,mimi nilidhani ni WASIRA.

    ReplyDelete
    Replies
    1. 1.Ulaaniwe wewe mwenye kufananisha binadamu na mnyama kwa chuki binafsi.
      2.''Hujafa hujaumbika'' kesho unaweza ukapata ajali ukaharibika sura kushinda hata huyo Wasira.
      3.Usimrebishe Mungu,hana makosa na hivyo ndivyo alivyopenda wasira awe,
      kwani ana tofauti gani na wewe unaejiona mzuri?kuna hitaji lolote unalolipata wewe tofauti na Wasira,kuwa na hofu ya Mungu.

      Delete
    2. MWENYEZI MUNGU KATUTOFAUTIFA BINADAMU NA WANYAMA,
      USIFANANISHE BINADAMU NA MNYAMA,HUKO NI KUMDHIHAKI MUNGU.
      TUBU!

      Delete
  2. kipi wanafanana na Wasira,Watu kwa kuropoka tu,kama huna comment piga kimya,

    ReplyDelete

Top Post Ad