Panya Wamla Mtoto wa Mwezi mmoja Vidole na Pua, Asubiria Upasuaji Kutengeneza Pua ya Bandia

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Taarifa kutoka mjini Johannesburg Afrika Kusini zinasema - kuwa panya walimng'ata mtoto wa mwezi mmoja vidole na pua Mtoto huyo anasubiri kufanyia upasuaji wa kuumba maumbile yake ya usoni baada ya tukio hilo huko Alexandra, Johannesburg .

Panya walimvamia Erena Yekanyi nyumbani kwao katika kitongoji duni cha Alexandra.
Wazazi wake wanasema kuwa hafana fulusi za kumpeleka hospitalini kwa matibabu anayohitaji kwa haraka baada ya kunga'twa jumatatu.
“nilikuwa nafua hapo nje naye Erena alikuwa ndani amelala.
Mara nikamsikia akilia ndipo nikakimbia ndani kuangalia kulikoni ,,,nilimpata anafuja damu ''alisema mamake Thandaza.
Sasa mtoto huyo anasubiri kufanyiwa upasuaji ambao utaumba upya pua lake na pia vidole vitatu vilivyong'atwa

Mamake anasema madaktari katika hospitali ya Charlotte Maxeke Academic Hospital wanasubiri achangishe pesa za kutosha operesheni hiyo.
Kulingana na ripoti hiyo tukio hilo sio la kwanza katika makazi hayo duni.
Inadaiwa kuwa watoto wengi na wazee wameripotiwa kung'atwa na panya hao wanaoonekana sio wa kawaida kutokana na kimo chao.
Msemaji wa mji wa Johannesburg Nkosinathi Nkabinde panya ni wengi katika mitaa hiyo kutokana na hali duni ya usafi.
Amesema kuwa kunamipango ya kuangamiza wanyama hao.

----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad