Papa wa Kanisa la Katoliki Amruhusu Padri Mosha Kuoa

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis amekubali kumuondolea sakramenti ya upadri, Raymond Mosha wa Jimbo Katoliki la Moshi ikiwa ni miaka 20 tangu padri huyo aombe kuachana na daraja hilo.

Barua ya uamuzi wa Papa Francis ilisomwa juzi katika parokia na vigango vyote vya Kanisa Katoliki Jimbo la Moshi katika ibada zilizofanyika katika makanisa ya jimbo hilo.

Miongoni mwa parokia ambazo barua hiyo ilisomwa ni Karanga ambako Paroko wake, John Matumaini alitoa tangazo hilo katika ibada zote. Uamuzi huo ambao ni nadra kutolewa na Papa, unamaanisha kuwa sasa padri huyo yuko huru kuoa na kuwa na familia.

Hata hivyo, wakati uamuzi huo ukitangazwa rasmi juzi, tayari Padri Mosha ambaye ni profesa wa falsafa na maadili katika Chuo Kikuu cha Nelson Mandela Arusha, ana mke na watoto watatu ambao kwa sasa wako vyuo vikuu.

Padri Mosha alisema aliandika barua kuomba kuondolewa daraja hilo mwaka 1994 kabla ya uamuzi kutolewa juzi.

Katika orodha ya mapadre 185 wa Kanisa Katoliki Jimbo la Moshi iliyopo katika tovuti ya jimbo hilo, jina la Padri Mosha linaonekana likiwa ni namba 23.

Akizungumzia hatua hiyo, Padri Mosha alisema: “Ninafurahi kufunguliwa kifugo hiki na hii itanifanya niishi kama Mkristo. Kwa vile hawajaniondolea sifa ya kutoa huduma kama vile ibada za mazishi, sakramenti ya mwisho na ubatizo, nitaendelea kutoa kwa wahitaji kwa sababu ninaupenda ukristo.

“Nashukuru sasa nimekuwa muumini wa kawaida nitaweza kufunga ndoa kanisani kwa kuwa nilikuwa nimefunga ndoa ya kisheria tu kwa DC.”
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

6 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. bora umekua mkweli hongera na mungu akubariki!

    ReplyDelete
  2. Basi mapadri wote waoe.

    ReplyDelete
  3. ulikua huna wito wa upadre ulitamani uzinzi wakati ulichagua maisha ya kitume na masharti yake unayajua nyinyi ndio wasaliti wakubwa hua mnapenda kuingia ktk maisha flani kwa kufuata mkumbo au cijui kulazimishwa sasa yalikushinda,uliomba uvuliwe upadre sababu ulijua ulichokifanya ulizini ukiwa padre ukazaa na watoto tena bila ndoa ivi ww ni mkristo gani jamani unazaa nje bila ndoa afu ukiwa ni mchungaji ukiwalinda kondoo wa bwana wasipotee,ivi ulikua unawafundisha nn waumini wako?hakika mbele za bwana utakua na hoja nyingi za kujibu maana umedharau daraja kubwa ulilokua nalo pia umemkana yesu na kutii amri za shetani....pumbavu kabisa ww....hata kama usingeomba kuvuliwa upadre bado ungetolewa tu sbb wakatoliki wapo strictly xana na sheria zao....

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ametubu,
      Mbinguni huwa kuna shangwe kubwa hata mtu mmoja kati ya 100 akitubu

      Delete
  4. wewe anony 11.59 usishangae wewe unayemhukumu huyu padre wetu mstaafu ukachomwa wewe yeye akaingia mbinguni. na sina uhakika sana kama unaelewa unachokiongea maana ungejua usingeropoka maneno yako hayo. huyo padre yuko sawa kabisa maana hajavunja amri yoyote maana ameoa kwa ndoa ya kwa dc na kama wewe ni mkatoliki kama mimi na umefungishwa ndoa ya kikatoliki utakuwa ulifundishwa kuw kanisa linaitambua ndoa ya bomani. think thrice meen before vomiting your words

    ReplyDelete

Top Post Ad