Diamond Kufanya Show ya bure Stuttgart, Ujerumani September 20 Kuwafidia Mashabiki

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Baada ya show ya Diamond Platnumz iliyokuwa ifanyike mjini Stuttgart, Ujerumani kushindwa kufanyika mwishoni mwa mwezi uliopita na kusababisha vurugu kutoka kwa mashabiki waliofika ukumbini kumshuhudia star huyo wa ‘Number 1′, show hiyo inatarajiwa kufanyika September 20, 2014 bila kiingilio.

Kupitia Instagram Diamond amethibitisha kwa kuandika:

“YES!!!! STUTTGART GERMANY!!! on this 20th of September 2014… kiukweli nilisikitishwa sana na kilichotokea last time Stuttgart… lakini baada ya kugundua kuwa pia lilikuwa ni kosa la mtu mwingine na si promotter kama nilivyodhani, yaani Brittis Events… ndipo tulipoamua na kuwaletea Burudani hii Mashabiki zetu pendwa wa Stuttgart….hakikisha ufikapo unapendeza zaidi maana kama ujuavyo safari hii Vyombo vyote vya habari ndani na nje ya nchi vitakuwa pale kwa RedCarpet…. kiingilio ni BUREEEEEE!!!… tafadhariwambie na wenzio wa nchi za karibu…#NORWAY #HOLLAND #SWITZLAND #BELGIUM #SWEEDEN na kadharika!!!!”
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

7 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Uwe mwangalifu Diamond! Shoo ya bure katika kumbi gani ya kuweza kuchukua kila mtu? halafu nani kakwambia itakuwa bure kabisa. Bure wewe uliyelipwa bila kufanya shoo?? Lakini gharama bado zipo tena za ukumbi Dj ulinzi nk. If the show was delayed because you wanted your pay upfront kiini cha makoza ni wewe...yule jamaa anaweza kukufanya mbaya... just saying!! Wee ungerudisha hela na kule usiende mpaka kupoe na kesi ya yule bwana iwe imeisha. Tena hana hata insurance ya kulipia uharibifu.. itachukua muda. Stay away from trouble sio kama waTZ wanaojua kusamehe na kusahau haraka hiyo kabila ingine mwanangu!!!

    ReplyDelete
  2. Ungekuwa unashaurika domo ungefanyia kazi ushauri WA mdau WA kwanza! Acha kabisa domo me c shabiki Wako lakini napenda nizidi kukuckia upo na afya na amani PIA! Achana na hiyo show inaweza kukuletea matatizo, unajuaje kama hasira zao zimekwisha? Na show yenyewe ya bure c itakuwa na wahuni watupu? Kuwa mwangalifu Sana mama yko bado anakuitaji na watanzania pia. Acha acha kabisa mdogo wangu.

    ReplyDelete
  3. Shule nzuriiii,eti show bureeeee we una Akili kweli????umeme,maji,heater,kulipa madj,ulinzi nk nani atalipa?usidanganye wajingaWajinga Wa bongo wasioelewa technology,

    ReplyDelete
  4. Kama ujawahi nyonyolewa vuzi bila kiwembe Haya,walisema watakutengua uboho polisi wamekusitiri.unarudi tena,au unadili la chini ya kapeti?

    ReplyDelete
  5. au zile vurugu zilikuwa za kutengenezwa kutafutia kiki?

    ReplyDelete

Top Post Ad