Diva Afunguka Tena…Adai Zitto Kabwe ni Mume Wake na Anatambulika Kisheria

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mtangazajiwa Kipindi cha Ala za Roho kinachorushwa kupitia Radio Clouds FM ya jijini Dar, Loveness Malinzi ‘Diva’ kwa mara ya kwanza, amejilipua kuzungumzia uhusiano wake na Zitto Kabwe kwamba walikuwa mke na mume.

Katika mahojiano maalum na mwanahabari wetu jijini Dar juzi, Diva alisema anashangazwa na baadhi ya vyombo vya habari  kumnyima uhuru wa kuongelea suala lake na ‘zilipendwa’ wake huyo wakati kisheria yeye ni mke wake hivyo anapaswa kuzungumzia kutengana kwao.

“Ninyi mnayaongelea mambo ya Zitto na mimi juu kwa juu tu hamjui kama mimi nimeishi naye kama mke na mume nyumbani kwake Masaki (Dar), sasa nini kilisababisha penzi letu kuvunjika watu hawajui, nina ushahidi wa kutosha lakini wanaongeaongea tu,” alisema Diva.Akaongeza: 

“Sasa ninavyojua mimi kwa sheria za nchi, mwanamke na mwanaume wakiishi pamoja kwa zaidi ya miezi sita tayari ni mke na mume. Hawezi kuniacha kirahisirahisi tu.”

Diva alikwenda mbele zaidi kufuatia kauli ya Zitto aliyoitoa hivi karibuni kupitia Kipindi cha Mkasi kinachorushwa hewani na Runinga ya East African Television ‘EATV’ na mtangazaji Salama Jabir.

Zitto aliulizwa ana uhusiano gani na Diva, naye akajibu ni mtu wanayefahamiana tu lakini si mpenzi wake.

Ilidaiwa kwamba, majibu hayo ya Zitto kwa Salama ndiyo yaliyoibua hasira ya Diva hadi kufikia hatua ya kutupia kwenye ukurasa wake wa Instagram, e-mail aliyodai aliwahi kutumiwa na Zitto siku za nyuma akimtaka asiwe anaweka wazi uhusiano wao kwa sababu atachafuka kisiasa.

-mail ilisomeka  hivi:
Unanikosea sana ujue unapoweka mambo yetu hadharani. Ninaonekana siwezi kuwa kiongozi kwa sababu nashindwa ku-handle masuala yangu binafsi.
“Madhara uliyoyafanya ni makubwa sana. Wapinzani wangu wa kisiasa watayatumia sana dhidi yangu.

“Ungekuwa unajua madhara yake usingethubutu kufanya ulivyofanya mara tatu sasa. Sijui nia yako nini, ila ipo siku utajua umenikosea sanasana.”
  
Swali la mwandishi:
Je, Zitto akikubali kufuata huo utaratibu uwe mkewe utamuacha GK ambaye umekuwa ukimtangaza kuwa mpenzi wako?
Diva: Hilo nitakujibu baadaye.

Siku za karibuni, baadhi ya vyombo vya habari vimekuwa vikiripoti uhusiano wa Diva na Zitto bila kuzama kwa undani.

Kufuatia Diva kutupia madai hayo mtandaoni na kudai yeye ana hadhi ya mke kwa Zitto na kauli ya Zitto kwenye runinga kwamba Diva si mpenzi wake, baadhi ya watu waliozungumza na Amani walionesha kwenda kinyume na mtangazaji huyo.

Wengi walidai kwamba wana kumbukumbu zilizonyooka kwamba Diva amewahi kujinadi kutoka na Mbongo Fleva, Gwamaka Kaihula ‘Crazy GK’.

“Sasa Diva anavyodai ni kama mke wa Zitto mbona anamtangaza mwanaume mwingine?” Alisema mkazi mmoja wa jiji aitwaye Yuda.

Naye Ismail Juma, mkazi wa Kigogo, Dar alisema aliwahi kusoma kwenye vyombo vya habari kwamba Diva anapumzika na mwanamuziki kutoka Kenya, Jackson Makini ‘Prezzo’ kiasi cha kumzalishia bifu na demu wa jamaa huyo, Huddah Monroe.
“Diva awe na aibu basi, asikurupuke wakati yeye mwenyewe si msafi kivile,” alisema Ismail.


Kufuatia madai hayo, kwa muda wa siku saba, Amani limekuwa likimsaka Zitto kwa njia ya simu lakini bila mafanikio.Watu wa karibu naye walipoulizwa alipo, walisema wanachojua ana shughuli zake nchini Zambia.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

10 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. kukaa na mme miezi sita sio kigezo cha kuitwa mke,labda kama hivi unavyoongea ungekuwa bado uko ndani kwa zitto .Kwani zitto hawezi kusema kuwa ulikuwa rafiki tu na kwamba ulikuwa nae wakati wa week end tu au siku mojamoja?
    kwani mna mtoto?au kwa sasa nini au kipi kitasimama kama ushahidi kuwa mlikuwa
    mkiishi pamoja zaidi ya miezi sita?hivi wewe ukiitwa mke na huyo aliyoko ndani
    kwa zito kwa muda huu tumuiteje?PUMBAFUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUU

    ReplyDelete
  2. Mi kunchoka huyu ntoto jemeni.........

    ReplyDelete
  3. Hivi huyo GK anajisikiaje ?

    ReplyDelete
  4. gk kalishwa lmbwta ndio maana kimyaaaaa. janamke kama hili hata kulala nalo ni aibu halijielewi sijui linavuta bang auuuu

    ReplyDelete
  5. Kwi kwi kwiiii kalishwa kinyeo plus.chizi kaanza karibu tutasikia kalazwa kichwa kinauma sijui cancer then giiiiii mwacheni alipuke kipande utamu

    ReplyDelete
  6. Nimesoma nae na kanizidi kidogo,lakini anavyojifanya mtoto wa 18,
    ananiudhiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii.ptuuuuuuuuuuu!

    ReplyDelete
  7. Bw. Mh.Zitto inaonekana umemkatisha penzi Diva
    maana bado anaweweseka kwa penzi lako.Vibaya hivyo wee kijana wa Kigoma!

    ReplyDelete
  8. hii story mbona diva ameikana jamani kujulikan ni tabu maan kun maudaku ya kupakaziwa kila day

    ReplyDelete
  9. ZITTO KAA KIMYA!

    ReplyDelete
  10. wewe zito alikuwa anakugonga tu, kelele za nini sasa?

    ReplyDelete

Top Post Ad