Fahamu Kilichomtokea Mtoto wa Jackie Chan Kufuatia Tuhuma za Kujihusisha na Dawa za Kulevya

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Polisi wa Beijing, China hatimaye wamemkamata rasmi mtoto wa mkali wa Martial Arts Jackie Chan anaefahamika kwa jina la Jaycee Chan kufuatia tuhuma za kujihusisha na dawa za kulevya.

Taarifa kutoka katika ofisi ya mwendesha mashitaka wa wilaya ya Dongcheng, zimethibitisha hatua hiyo ambapo Jaycee Chan anaweza kufungwa hadi miaka 3 jela endapo atakutwa na hatia ya kuwaruhusu watu kutumia dawa za kulevya katika nyumba yake.

Jaycee Chan alikamatwa mwezi uliopita akiwa na muigizaji mwingine wa Taiwan anaefahamika kwa jina la Ko Kai. Wawili hao walifanyiwa vipimo na kugundulika kuwa walitumia dawa za kulevya aina ya Marijuana na walikiri kuwa walipeleka nyumbani kwa Jaycee grams 100 za dawa hizo.

Kwa sheria za China, Polisi anatakiwa kuomba ruhusa ya kumkamata rasmi mtuhumiwa kutoka kwa muendesha mashitaka wa serikali. Taratibu za upelelezi zinaweza kuendelea wakati huo.

Kwa upande wa Ko Kai, alipewa kifungo cha siku 14 baada ya kukiri kutumia marijuana na baadae yeye na familia yake walifanya mkutano na waandishi wa habari na kuomba radhi kwa kitendo hicho.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad