Sugu na Jide ni Wasanii Wasioguswa, Ukiwagusa Umepotea Kimoja, Pitia Hapa Ushuhudie

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

1. Lady Jaydee

Uyu dada ndio msanii mwenye washabiki kuliko wasanii wote Bongo, ni mwanamuziki anayeheshimika na wasanii wenzake karibu wote na wadau mbalimbali wa muziki na sekta zingine.

Aliyejaribu kumgusa Msanii yoyote anayejaribu kumgusa uyu dada unapotea yeye, wasanii waliioonja joto ya Jide ni awa wafuatao na wakapotea

Chidi benzi;
uyu baada ya kuvuma sana akawa anamchokoza uyu dada kwa kufanya mambo ya kumkosea heshima Komando leo amebakia hadithi, ameishia kuwa mteja.

Mwana FA;
uyu alikuwa rafiki mkubwa wa Jide na alimshirikisha Jide kwenye album zake zote, ata maisha ya kawaida walikuwa wakishirikiana kwenye vingi.
Mwishoni alikuja kumsaliti Jide kwa kutumika na Joseph Kusaga na Clouds kujaribu kudhoofisha mahudhrio ya show ya Jide ya kutimiza miaka 10, hii ilizua ugomvi mkubwa kati yao na baada ya hapo FA akapoteza mashabiki wake wengi sana waliomchukulia kama msanii mwenye upeo mkubwa.
Ana wimbo mpya mkali sana ‘mfalme’ ila umepotea kwa kuwa FA ameshatoka mioyoni mwa watu.

Mrisho Mpoto

Msanii uyu wa ushahiri alijiharibia baada ya kumtaka Jide amkabidhi kijiti Lina au Recho wakati wake umepita, na aliyazungumza haya kwenye jukwaa la fursa.
Baada ya hapo waliomchukulia kama mwanaharakati ambao ndio walikuwa washabiki wake wakubwa wakambeza na kumpotezea moja kwa moja.
Mpoto amebaki kupata matangazo ya serikali ila muziki umeisha na ataki kukabidhi kijiti kwa Mpoki wanaefanya style moja kama alivyomtaka Anaconda.

Ben Pol
Uyu alimwita Jide mgonjwa wa akili kupitia social networks, baada ya Jide kumtuhumu kuvunja mkataba wa kutumbuiza show yake ya kutimiza miaka 10. Kwa sasa Ben ni hadithi iliyopita.

Wapo wengi wengine ni ishu za chini ya kapeti


MR II Sugu aka Nyerere wa Rap

Uyu ndio baba wa Bongofleva na hiphop kwa ujumla. Ni msanii anayeheshimika kwa misimamo yake ‘tata’ na uwezo wa kupambania mambo mbalimbali. Historia na mchango wake kwenye muziki wa Tanzania hakuna anayeweza kumnyang’anya japo kuna waliojaribu ila wakashindwa.
Kwa sasa ameeegemea zaidi kwenye siasa, akiwa kama mwakilishi wa watu wa Mbeya mjini.

Waliomgusa

Mwana FA

Uyu FA alikuwa rafiki mkubwa wa Sugu, aligeuka adui baada ya FA kujigeuza ngao kwenye ugomvi wa Sugu na Clouds media akisimama kati kumzuia Sugu asifikishe makombora yake kwa upande wa pili (refer AntiVirus Saga). Tangia hapo FA alijipoteza ushawishi na zaidi baada ya kuharibu na kwa Jide, akajibrand upya kama kibaraka.

Roma Mkatoriki

Uyu alimdiss Sugu kwenye wimbo wake wa KKK na ukawa ndio mwisho wa Roma. Kwa sasa anatoa ngoma zinabaki kuwa habari tu kuwa Roma ametoa mpya ila zinabuma.

Bwana Misosi

Alimdiss Sugu kwenye kwenye ‘nitoke vipi’ na akafanikiwa kuvuma kwa muda . Ingawa alikuja kusahihishakauli lakini alipotea yeye akamwacha Sugu aliyemkashifu .

Joh Makini

Kwenye wimbo wake ‘ manuva’ alimdiss Sugu akisema anafanya harakati magirini. Kwa sasa Joh anasafiria nyota ya weusi maana nyimbo anazotoa baada ya hapo zinabuma.

Kuna wengine wengi tu kina Afande sele, Mox, Jafarai na wengineo wote waliomjaribu Sugu wamepotea.

Kifupi hakuna aliyewahi kuwagusa awa manguli akabaki salama.

Swali ni je, Kwa nini imekuwa hivi?

Written By  Mr Gentleman
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Wewe Mr. Gentleman uliegundua hilo ndio unaepaswa kutuelezea ni kwanini imekuwa hivi.

    ReplyDelete
  2. Mr.Gentleman,HUNA JIPYA !
    Kwendraaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa

    ReplyDelete
  3. Jide mkali sana na anajua anchofanya kwa ufupi hakurupuki!!!

    ReplyDelete
  4. siku zote ukimuwazia mwenzako mabaya au ukinena ubaya juu ya mwenzako siku zote hugeuka baraka juu yake na yale maneno hukurudia we uliesema ....xo hapo hamna ndumba wala nini?big up jideeeeeee siste wa ukweeeee.........................................

    ReplyDelete
  5. tatizo udaku na wenyewe huwa wanadanganya... tusiwaamini sana

    ReplyDelete

Top Post Ad