Tuzo aliyojipa H.Baba ‘Mtumbuizaji Bora’ ni diss kwa Diamond Platnumz?

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Pamoja na H.Baba kuwahi kudai kuwa hana tena beef na Diamond Platnumz, kuna kila ishara kuwa mafahari hao wawili bado hawawezi kukaa kwenye zizi moja. Kama umesahau, wacha tukukumbushe; Wasanii hao wawili wamewahi kuingia kwenye beef zito baada ya H.Baba kumtuhumu Diamond amemuibia wimbo wake ‘Sitaki Kulewa’.

So, Jumamosi iliyopita, H.Baba na mke wake, Flora Mvungi waliandaa tuzo zao wenyewe ambazo tofauti na vile wengi wanavyodhani, tuzo hizo zilikuwa serious kabisa kwa kuhusisha watu muhimu kwenye tasnia ya burudani Tanzania, waandishi wa habari na pia kutolewa trophy na fedha taslimu kwa washindi.

H.Baba alijipa tuzo ya ‘Mtumbuizaji Bora’ na tunafahamu kuwa Diamond Platnumz ni mshindi wa kipengele cha ‘Mtumbuizaji bora wa kiume wa muziki’ kwenye tuzo za KTMA 2013. H.Baba anataka title yake kutoka kwa Diamond?

Haya ni maneno aliyosema wakati akipokea tuzo hiyo:

Tuzo hii hapa ni ya mtumbuizaji bora Tanzania,” alisema muimbaji huyo. “Mimi nina tuzo ya East Africa mtumbuizaji bora, Tanzania sina hata tuzo moja kwa sababu ya nini nimeshatangaza naanzisha hii tuzo kwa akili timamu na wala sivuti bangi. Mimi sivuti sigara wala sinywi pombe, kama kuna msanii anaona hii tuzo sio halali yangu mimi ajitokeze. Promota yoyote ajitokeze huyo msanii alipwe pesa mimi nita- perform bure na awadhihirishie watanzania kwamba yeye ni mkali ya stage Tanzania.

Kama ananizidi mimi, promota amlipe yeye ila mimi kama H.Baba nitaperform bure na nitakuja peke yangu na yeye inatakiwa aje peke yake. Kwa sababu kuna Kiswahili fasaha ambacho kinakosewa kuna neno linaitwa mtumbuizaji bora na kuna watumbuizaji bora. Mimi ni mtumbuizaji bora, wengine ni watumbuizaji bora. Kwanini nasema watumbuizaji bora kwa sababu msanii yeye mwenyewe hajiwezi mpaka awe na watu wakucheza naye, ila mimi binafsi najiweza kwa sababu mimi mwenyewe ninaweza fanya kazi na ikaeleweka.

Ndiyo maana ya hii tuzo niliyopata leo. Ninaowatambua walikuwa watumbuizaji na ninawaheshimu mpaka leo nawataja watu wawili, kuna Mr Nice kuna TID (Top In Dar ) hao ndo watu wanaweza kusimama kwenye show na kuburudisha na watu wakasema asante.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

10 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hahahhahahaha,na hao uliowataja wote mnafanana akili,yaani hujakosea bro.

    ReplyDelete
  2. chizi mbwa ww umepotea sasa unalazimisha kurudi kweny level yako uliyokuwa nayo kila nabii na wakati wake mwache mtoto wa watu atambe. unavomsakama pengne ata maji yanampalia akinywa .cha msingi lea uyo mtoto wenu usije ukambemenda tanzanite sijui pengine aje kumshusha diamond maana wote ni madini adimu tanzania

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kwani aliloongea la uongo hapo ni lipi?? Diamond peke yake kwenye stage hajiwezi na huo ndo ukweli japokuwa unauma kwake yeye na sisi mashabiki wake... Jamaa kaongea ukweli

      Delete
  3. Sifa nzuri ni ya kusifiwa, sio ujisifu mwenyewe.
    Huyo unayemponda saa hizi yupo ughaibuni anadatisha watu, wewe je?
    'KALAGABAHO NA UBOZI WAKO'

    ReplyDelete
  4. kwa wimbo upi h mama!hahahahaha

    ReplyDelete
  5. Labda kukata mauno mbele ya kadamnasi ndio kutumbuiza sawa,wote wa2 sijawaikuona kuwa ni watumbuizaji.

    ReplyDelete
  6. kaka achana na huyo mtoto "diamond" utaumbuka..wewe humuwezi huyo.

    ReplyDelete
  7. Mhh hapo umechemsha h.baba,daimond anaimba na kucheza pia ingawa ana madancer wake lkn anajua kucheza pia,tn ni mbunifu sasa wewe ukiwa stajini ni kukata mauno mwanaume mwanzo mwisho,,tunataka vitu tofauti bn mauno kdg ngololo kdg basi burdaaaaan.Cheza mbali kbs na daimond ww humfikii miaka800000.yani umekaa huko na mkeo mkasema ngoja mumkomeshe daiiii!!!!!hahahaa poleni

    ReplyDelete
  8. Kama umeamua hivyo c kimpango wako kuna haja gani ya kuongea majungu kwenye kadamnasi ya watu unajinyesha ulivyo na akili ndogo km uliowataja bangi tupuau unatafuta kiki!!

    ReplyDelete
  9. Huna point kwa kweli kaa kimya subiri kusifiwa we baba haaaaaah

    ReplyDelete

Top Post Ad