Mwanamuziki Chid Benz Kuendelea Kunyea Debe Mahabusu, Aingia Mahakamani Kavaa Mlegezo

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

MSANII wa Muziki wa Kizazi Kipya (bongo fleva), Rashidi Abdallah Makwaro (29), maarufa kama Chid Benz, amefikishwa mahakamani akikabiliwa na mashitaka matatu ikiwemo kukutwa na Dawa za kulevya aina ya Heroin yenye thamani ya Sh. 38,638, bangi ya Sh. 1,720 na vifaa ya kuvutia dawa hizo kijiko na kigae.
Chid Benz amefikishwa  mapema leo saa 3:00 asubuhi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kusomewa mashitaka yake. Saa 7:50 mchana alifikishwa mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Warialwande Lema aliyepangiwa kusikiliza kesi hiyo.
Hata hivyo, hakimu aliamuru msanii huyo kutolewa nje ili akave vizuri nguo baada ya suruali aliyokuwa amevaa mlegezo maarufu kama kata kei kuonyesha nguo yake ya ndani.
“Kwanza mtoeni nje aende akavae nguo hizo zinazodondoka…” aliamuru Hakimu.
Saa 7:54 alirejeshwa ndani ya chumba cha mahakama upande wa Jamhuri ukiongozwa na Wakili wa Serikali Mwanaamina Kombakono akisaidiana na Inspekta Jackson Chidunda, ulimsomea mashitaka yake.
Wakili Kombakono alidai kuwa Oktoba 24, mwaka huu katika uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere, uliopo Ilala jijini Dar es Salaam, mshtakiwa alikutwa dawa za kulevya aina ya heroin isivyo halali zenye uzito wa gramu 0.85.
Katika shitaka la pili, ilidaiwa kuwa siku na eneo la tukio la kwanza, mshtakiwa alikutwa na gramu 1.72 za bangi isivyo halali.
Wakili huyo wa serikali alidai kuwa, siku na eneo la tukio la kwanza na la pili, mshtakiwa alikutwa akiwa na vifaa vinavyotumika kuvua dawa za kulevya aina ya heroin, kigae na kijiko huku akijua ni kosa.
Mshtakiwa alikana mashitaka yote na upande wa Jamhuri ulidai kuwa hauna pingamizi na dhamana dhidi ya mshtakiwa.
Hakimu Lema alisema mshtakiwa atakuwa nje kwa dhamana kwa masharti ya kuwa na wadhamini wawili wanaotoka kwenye taasisi zinazoamini na siyo walimu na dhamana ya Sh. Milioni moja.
Hata hivyo, mshtakiwa alishindwa kutimiza masharti hayo na amepelekwa mahabusu hadi Novemba 11, kesi hiyo itakapotajwa.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

7 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. huyu jamaa bwege kweli, mwache apate mvua za kutosha ili iwe fundisho kwa hapa vijana vichwa maji wasasa hivi!! pumbaf!!

    ReplyDelete
  2. pole kaka, na wewe hapo juu msenge sana, hebu vikiria angekuwa ndio wewe au ndugu yako pamoja na kosa hilo ungependa akafungwe ? hebu kuwa na akili wewe

    ReplyDelete
    Replies
    1. wewe ndo mavi kweli, au na wewe ni teja unatetea uhanisi, bwege wewe na wewe ukamatwe ule mvua nyingi, nyie vijana wa siku hizi mabwege sana, mnaiga vitu nje kabisa ya maadili yenu, pumbaf!!

      Delete
    2. we mbilikimo unataka matusi eti angekuwa yeye au ndgugu yake.. Elewa kwanini kasema hivyo kwa maana siyo yeye mtu anayejijuwa hawezi kutumiaunga au bangi tena na kupita navyo sehemu ka za uwanja wa ndege kama vile... mtu anayejifanya muimbaji na maarufu tanzania mpaka kufikia kuamuwa kupita na unge namna ile uwanjani kwa kujiamini amwkosa dhamana ya milioni moja na watu wawili wa taasisi inayojulikana kweli? unachomtetea kitu gani? samahani kwa hili ngoja nikuambie tu chid benz lazima atakuwa anakufira wewe na mama na baba yako na ada zako woote.. kenge we.

      Delete
  3. jamaa ale mvua kwa faida yake,na wewe hapo juu msenge vile vile.unatetea ujinga akikaa ndani atakosa unga na akitoka atajirekebisha,jamaa ameshakua teja kwa wale wanaomjua wameshaliona tatizo

    ReplyDelete
  4. bado wengine watakuja tu....... mziki mmoja unamiliki gari hatareeeeeeeeee"""" ni sheeeeeeda! wasanii badilikeni

    ReplyDelete
    Replies
    1. na dhamana ya milioni moja katolewa na mama yake hahahahahahahahah

      Delete

Top Post Ad