TBC Yashika Nafasi ya Mwisho Kuangaliwa na Wananchi

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Kwa hali ya kushangaza, kituo cha television cha matangazo cha tbc 1 kati ya vituo vinne maarufu vya matangazo ya habari nchini Tanzania kimeshika nafasi ya mwisho baada ya kufanyiwa utafiti,

Kwa habari za uhakika ni kwamba kituo kilichoongoza kuangaliwa na watazamaji wengi ni ITV kikifuatiwa na Star TV, nafasi ya tatu imeshikwa na Channel 10 na hatimaye TBC1.

Kwa utafiti uliofanya na na TCRA imebainika kuwa ni aibu kama kituo television ambacho ni cha Taifa na ni UMMA kushika mkia nyuma ya vituo binafsi jambo ambalo ni hatari.

Vyanzo vya kuaminika vinadai kuwa TBC1 imefikia hapi baada ya kugundulika inabagua baadhi ya habari ya vyama vya siasa na kutoa habari ya chama kimoja tuu jambo ambalo siyo sahihi katika utashi wa utangazaji na kutofuata uhuru wa kiutangazaji ndani ya uongozi wa shirika la habari la Tanzania, 

Utafiti umeonyesha kuwa ili chombo cha habri kiweze kuangaliwa na watu wote wa vyama vyote ni lazima chombo cha habari kitoe habari bila kubagua vyama vya siasa maana watazamaji wana misimamo tofauti na itikadi tofauti, na kama chombo cha habari kikiamua kutoa habari kwa chama kimoja cha siasa basi ujue hapo watakaoangali hizo taarifa za habari ni hao hao wa chama kimoja.

Watafiti pia walienda mbali zaidi na kukinyoshea vidole kituo cha taifa cha utangazaji kuwa ni chombo cha UMMA na kisipende kubagua baadhi ya taarifa za habari za vyama vya siasa kwa misingi ya kuelekezwa na wanasiasa au viongozi wa nchi maana madhara yake ni wananchi kushindwa kuangalia hicho kituo.

Mwisho wake kitashindwa kufanya biashara na hatimaye kutegemea tuu ruzuku serikalini na hapo ndo nchi itazidi kupata hasara badala ya kukiacha chombo kijiendeshe kwa uhuru. Wametoa mfano kama shirika la habari la Uingereza BBC lingefanya kama TBC inavyofanya basi nayo ingeishia kutazamwa tuu nchini uingereza na tena kwa watu wachache tofauti na ilivyo sasa BBC inatazamwa duniani kote.

Utafiti umeonyesha kuwa hivi vyombo vingine vya habari ITV, Star TV na Channel 10 vimepata watazamaji wengi kwa kuwa havibagui matangazo ya kada tofauti ya vyama vya siasa na hapo ndoo inasababisha waweze kupata watazamaji wa kutosha.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. sababu ni radio ya ccm, ndo maana hatuna habari nayo!!!

    ReplyDelete
  2. Yaan cku ya chanjo surua ndo ilikua balaa mana ckuona jipya mwanzo mwisho chanjochanjo aisww TBC INACHOSHA

    ReplyDelete
  3. TANZANIA BROADCAST CCM = TBC

    ReplyDelete
  4. hivi hii bado iko, mi nilishaidelete kabisa, mimi na familia yangu woooooote hakuna kuangalia upuuzi huu, ngoja waje wachukue nchi upande wapili sijui mtafanyaje?anyway tutaiuza kwa wanaojua bishara wawekeze, na wote waliohusika tunawastaafisha kwa manufaa ya umma , na wengine tunawapeleka mahakamani kwa ufisadii, naju upo mwingi tu hasa hizo ruzuku

    ReplyDelete
  5. inabidi waliangalie upya hilo shirika maana sijeikawa kama RTD HIVI IPO AU MAANA SINA UHAKIKA

    ReplyDelete

Top Post Ad