Nahodha wa Bafana Bafana Senzo Meyiwa aliuawa akimuokoa mpenzi wake

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Nahodha wa Bafana Bafana na Orlando Pirates Senzo Meyiwa aliuwa kwa risasi na majambazi alipokuwa akijaribu kumlinda mpenzi wake walipokuwa nyumbani kwa mpenzi wake huyo, karibu na Johannesburg, maofisa wamesema leo.

Mlinda mlango huyo wa Orlando Pirates aliuawa jana baada ya kupigwa risasi kifuani mbele ya mpenzi wake ambaye ni muimbaji na muigizaji. Katika tukio hilo, watu wawili waliivamia nyumba hiyo liyopo katika mji wa Vosloorus na kutaka wapewe simu, fedha na mali zingine.

“Senzo alitaka kumlinda Kelly sababu mmoja wao alikuwa amemwelekezea bunduki,” afisa mmoja aliwaambia waandishi wa habari. Polisi wanadai kuwa siku ya jana watu watu wawili waliingia nyumbani kwa Khumalo saa mbili usiku huku mwingine akisubiri nje na walipomaliza walikimbia.

Orlando Pirates,  imeandika kwenye Twitter: “@Orlando-Pirates family has learned with sadness of the untimely death of our number 1 keeper & captain Senzo Meyiwa.

Irvin Khoza, mwenyekiti wa club hiyo ameongeza: “This is a sad loss to Senzo’s family especially his children, to Orlando Pirates & the nation.”
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad