Wabunge Tisa Wajiuzulu Kumpinga Shy-Rose

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mgogoro ndani ya Bunge la Afrika Mashariki (Eala) umechukua sura mpya baada ya wabunge tisa, wakiwamo makamishna watano na wenyeviti wanne wa kamati za Bunge hilo, kuwasilisha barua za kujiuzulu nafasi zao hizo, ikiwa ni matokeo ya sakata linalomhusisha mbunge mwenzao kutoka Tanzania, Shy-Rose Bhanji (pichani).

Kutokana na hali hiyo, Bunge hilo ambalo lilikutana kwa wiki mbili huko Kigali, Rwanda liliahirishwa jana kwa muda usiojulikana, muda mfupi baada ya kushindwa kufanya uamuzi wa kumwadhibu Bhanji ambaye anakabiliwa na tuhuma mbalimbali za utovu wa nidhamu.

Mgogoro huo ulisababisha Eala kwa wiki mbili, kushindwa kufanya lolote lililokuwa limepangwa kwenye kalenda yake, kwani kila lilipokutana, wabunge walitoa hoja liahirishwe hadi pale suala la nidhamu dhidi ya Bhanji litakapotolewa uamuzi.

Mbunge huyo anatuhumiwa kutoa maneno yasiyokuwa na staha kwa wenzake, kuwakashifu na kuwatukana baadhi ya viongozi wakuu wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, wakati wa ziara ya ujumbe wa Eala katika nchi za Jumuiya ya Ulaya (EU), Ubelgiji.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. MBONA HABARI YENYEWE HAISEMI NANI KATUKANWA NA HIZO FUJO ALIZOFANYA KWENYE NDEGE MPAKA KAFUNGWA PINGU TUONYESHWE KAMA NI KWELI

    ReplyDelete
  2. KWA MTAZAMO WANGU NAONA KUNA AJENDA YA SIRI SHY ROSE SIMAMIA UKWELI KAMA UMEFANYA HAYO ACHIA NGAZI

    ReplyDelete
  3. Eti 'hafukuzwe' (afukuzwe) 'hakumbuke' (akumbuke) 'staa' (staha) rudi darasani (la kwanza) utafundishwa kutamka maneno vizuri.

    ReplyDelete

Top Post Ad