Uchaguzi wa serikali za mtaa: Wakurugenzi Watano Wafukuzwa Kazi

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Serikali imetengua uteuzi wa Wakurugenzi sita wa Halmashauri, na kuwasimamisha kazi wengine watano kupisha uchunguzi, kutokana
na kubainika kuchangia kuvurugika kwa uchaguzi wa Serikali za Mitaa, uliofanyika tarehe 14, mwezi huu.

Akitangaza hatua hiyo kufuatia ripoti iliyoibua madudu yaliyofanyika katika uchaguzi huo Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Hawa Ghasia amesema uamuzi huo pia umeridhiwa na Rais Jakaya Kikwete.

Mhe. Ghasia amewataja halmashauri ambazo wakurugenzi hao waliotenguliwa uteuzi wao kuwa ni za Mkuranga, Kaliuwa, Kasulu,
Serengeti, Sengerema na Bunda, waliosimamishwa kazi ni wakurugenzi wa Hanang', Mbulu, Ulanga, Kwimba pamoja na wa Manispaa ya Sumbawanga.

Waziri Ghasia amesema kuwa Wakurugenzi wengine watatu wapewa onyo kali, ambao ni wa Rombo, Busege na Muheza na wengine
watatu wakipewa onyo la kawaida, wakurugenzi hao ni wa Manispaa Ilala, Hai na Mvomero.

MY TAKE 
mwaka huu kila mtu atakuwa mamluki nabadooooo
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad