Utabiri wa Urais 2015, Mgombea Kufa Akitafuta Urais 2015

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mrithi wa Mnajimu na Mtabiri wa Afrika Mashariki, Kati na Kusini, Marehemu Sheikh Yahya Hussein, Alhaj Maalim Hassan Yahya Hussein, ametabiri kwamba kiongozi mmoja mzee aliye kwenye kinyang’anyiro cha kuwania urais, atadondoka ghafla kwenye jukwaa na kufa mwakani.

Amesema kiongozi huyo, ambaye hakumtaja jina, atafariki dunia baada ya tukio hilo wakati akikimbizwa hospitali.

Alitangaza utabiri huo, alipozungumza na waandishi wa habari, jijini Dar es Salaam jana, kuhusu kutumia kwa utabiri alioutangaza mwaka 2014, uchaguzi mkuu na utabiri wa mambo mbalimbali yatakayotokea mwaka 2015.

“Kiongozi mmoja mzee kwa umri ambaye yumo kwenye sakata la urais atadondoka ghafla kwenye jukwaa na kufa akikimbizwa hospitalini,” alisema Maalim Hassan.

Pia alisema kwa mwaka mpya wa 2015 kuanza siku ya Alhamisi, kunaashiria wazee maarufu na hasa wale walio katika uongozi au waliokuwa viongozi kufariki kwa wingi na kwa hilo akasema: “Mtaona ajabu yake.”

Vilevile, alitabiri mwaka 2015 kwamba utakuwa wa shida kubwa kwa familia, ambazo iwapo wahusika hawatafanya juhudi za kuangalia watoto wao, vifo vya ajabu vitatokea ndani ya familia zao.

Pia alitabiri mwaka 2015, wizi utakuwa mwingi na wezi watauawa na udhalimu wa madhalimu utabainika na kuumbuka.

Aidha, alitabiri mwaka 2015 kushuhudia uongo mwingi wa kutisha hasa kutoka kwa viongozi wa kidini na kisiasa pamoja na wanawake wenye nyadhifa au maarufu katika jamii

Pia alitabiri mwaka 2015 utamweka wazi kiongozi mmoja mashuhuri wa siasa nchini kurukwa kwake kwa akili bila kufichwa au kusitiriwa kama ilivyokuwa katika mwaka 2014.

Alisema katika mwaka 2014, kiongozi huyo alikumbwa na mkasa huo, lakini suala hilo likafanywa kuwa siri kubwa.

Pia alitabiri misiba miwili ya kitaifa kutokea nchini mwaka 2015 kwa mujibu wa nyota na kwamba, kuna kiongozi mmoja wa kidini atakumbwa na kashfa ya mwaka itakayomsababishia anguko kubwa na la aibu.

Kadhalika, alitabiri viongozi wawili wa siasa na dini kwamba watakumbwa na kashfa ya ngono, ambayo itawasababishia anguko la utumishi wa kutukuka na familia zao.

Pia alitabiri mwandishi mmoja mashuhuri nchini atakumbwa na umauti wa utata utakaoitesa serikali na familia yake kutafuta suluhu.

Alisema mwaka 2015 utakuwa wa viongozi kuzama kisiasa na kukumbwa na kashfa kubwa zitakazowaondoa madarakani, ikiwa na maana kwamba viongozi wanaofahamika wataanguka kiuchumi, kisiasa, kibiashara na kijamii.
~Nipashe
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. mmmmh MAKUBWA.......MUNGU TUSAIDIE WATANZANIA WOTE

    ReplyDelete

Top Post Ad