Zamaradi Apewa za Uso Baada ya Kushikilia Bango issue ya Filamu za Bongo Kupunguzwa Bei

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Wadau, muhindi 'steps entertainment' wameshusha bei za filamu zao kutoka shilling elfu 3 mpaka shilling 1500.

Huyu muhindi ni mfanyabiashara kama alivyo Joseph Kusaga wa Clouds, anaamua hela ya kuuza films kama anavyoamua Kusaga na Ruge bei za kuwalipa wasanii wanavyopanda show za fiesta. 

Cha kushangaza Zamaradi mketema amemshikia bango muhindi mpaka kwenda kumsemea kwa 'baba'. Hii ishu ameigeuza maada kuu kwenye Clouds . Anapinga muhindi kushusha bei ya filamu za kibongo eti itaua soko la filamu. Itaua soko la filamu au itaua kikampuni chake cha kwenye bahasha?? Anawalaumu kina JB kwa kusimama upande wa Steps, kina JB wanakosa gani si wanaangalia maslahi yao? kama yanafikiwa kwa nini wasimsapoti muhindi! Hii ni kama tu wale wasanii wanaopanda steji ya fiesta kwa laki moja ilihali Kusaga anatengeneza billions kutumia wao. 

Amefikia mbali kiasi cha kuitupia lawama BASATA eti hawana wanachofanya eti hawana msaada, watafanya nini na nyie ndio wa kwanz! kuwadharau, juzi tu hapa waliwapa amri msimtumie Davido na kuwaonyesha dharau mkamtumia bila wasiwasi wowote. Leo ndio unajua umuhimu wa Basata!? 

Zamaradi na watu wako nawashauri acheni kupiga kelele, mwacheni afanye biashara yake as long as hajavunja sheria yoyote. Kwanza ni mlipa kodi mzuri sana kuliko vikampuni vyenu vya mfukoni.

Pili, hamna filamu za kutuuzia raia shilling elfu 3 mia tano. Mnatuibia sana sababu hizo filamu zenu hazina quality hata ya kutuuzia elfu moja.

Zamaradi nakushauri acha kelele, shindana kihalali kama unataka kuingia kwenye hii biashara vizuri. Usitumie power ya media yenu kuingilia biashara za wengine.

~Source:Jamii Forums
By Mr gentleman
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad