Ajifungua Watoto Mapacha Walioungana Katika Eneo la Kifua

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mwanamke mmoja mkazi wa Kata ya Buhare katika Manispaa ya Musoma Mkoani Mara, Helena Paulo (20), amejifungua watoto wawili mapacha ambao wameungana katika eneo la kifua hadi tumboni tukio ambalo limevuta hisia za mamia ya wananchi ambao wamefika katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa huo kwa lengo la kutaka kushuhudia tukio hilo.

Akizungumza katika wodi ya wazazi katika Hospitali hiyo Muuguzi wa zamu, Naabu Geraruma, amesema kuwa mwanamke huyo amefanikwa kujifungua Januari 5, 2015 usiku wa saa saba kwa njia ya operesheni ambapo watoto hao wenye jinsi ya kike wamezaliwa wakiwa na uzito wa kilo 4.6.


Amesema tukio hilo ni la kwanza kutokea katika Hospitali hiyo na kwamba hali ya mwanamke huyo na watoto zinaendelea vema na taratibu za kumpeleka katika Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Mwanza Bugando zimekamika.

Taarifa kutoka jijini Mwanza na kuthibitishwa na Mkurugenzi wa Utawala na Rasmali Watu wa hospitali hiyo, Leah Kagine, zinasema tayari mwanamke huyo na watoto wamefikishwa katika hospitali hiyo kwa ajili ya matibabu na uchunguzi zaidi.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad