Chenge Ageuka Mbogo Bungeni baada ya kuitwa FISADI.......Amtaka Halima Mdee Atoe Ushahidi Kuthibitisha Kauli yake

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

MBUNGE wa Kawe, Halima Mdee (Chadema) ametakiwa kuwasilisha ushahidi kuthibitisha kauli yake ya kumtuhumu Mbunge Bariadi Magharibi, Andrew Chenge (CCM), kwa ufisadi.

Chenge alilazimika kuomba utaratibu wa kiti juzi, baada ya Mbunge huyo wa Kawe kumtaja mara mbili wakati akichangia mjadala wa taarifa za kudumu za Bunge zilizowasilishwa juzi.



Mara ya kwanza, Mdee alimhusisha Chenge na mkataba mbovu wa Kampuni ya Ndege (ATCL) uliosababisha Serikali kuingia hasara ya zaidi ya Sh bilioni 90.

Licha ya kumtaja kwenye ufisadi huo ambao kwa mujibu wa Mdee, Chenge ndiye alikuwa Waziri wa Wizara yenye dhamana na ATCL, pia alimtaja kuhusika katika kashfa nyinginezo ikiwemo suala la utoaji takribani Sh bilioni 200, katika iliyokuwa Akaunti ya Tegeta Escrow ya Benki Kuu (BoT).

“Wabunge tuanze kuchunguzana humu ndani na kushughulikiana,” alisema Mdee na kutaja kwamba kwa kuanza, waanze na Chenge pamoja na Dk Shukuru Kawambwa (Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi), akimhusisha kuwa aliwahi kushika wizara hiyo yenye dhamana na ATCL.

Kauli hiyo ilimfanya Chenge kusimama na kusema; “kwa heshima zote nimemvumilia sana mheshimiwa (Mdee) anayechangia hoja hii. Kama ana ushahidi wa hayo anayosema, kanuni zetu zinatutaka ayawasilishe mbele yako.

Mimi ningelipenda Bunge hili liendelee kuwa na heshima yake. Pili naomba sana, hayo wanayoyasema wawe na ujasiri wa kwenda kuyasemea nje ya ukumbi huu wa Bunge, wasijifiche kwenye kinga ya Bunge.

 “Nina mengi ya kusema, lakini kwa sababu nimesimama kwa hoja ya utaratibu, kunitaja moja kwa moja, naomba aweke hoja mezani,” alisema Chenge.

Mwenyekiti wa Bunge alikubaliana kwamba Mdee awasilishe ushahidi kwa kiti. Hata hivyo Mdee alijibu, “Kuna utaratibu wa kikanuni, vielelezo nikitakiwa kuleta nitaleta.

"Tunazungumza hapa matumizi mabovu, mikataba mibovu na wizi wa mali ya umma. Mzee wangu (Chenge) ni rafiki yangu lakini nimeamua nimfungukie kwa sababu haya ni mambo makubwa.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Ili kudhibitisha kuwa hawa ni wanasiasa tu na hawana hoja zozote za kimsingi zaidi ya ngonjera. Yafuatayo ndio maneno yao "Mzee wangu (Chenge) ni rafiki yangu" mwisho wa kunukuuu. Kweli kwa staili hii tutafika kweli??????? TUMECHOKA NA NGONJERA ZENU. Kama hamuwezi kuchukua hatua zozote za maana dhidi ya mafisadi KAENI KIMYA.

    ReplyDelete
    Replies
    1. sasa we ulitaka asemeje?na ndo kesha muwasha,ebo!

      Delete

Top Post Ad