Muuza Genge Achezea Kichapo kizito baada ya kunaswa na Mke wa Mtu

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Muuza genge mmoja kwenye Soko la Mji Mpya mjini Morogoro ambaye jina halikupatikana mara moja, amejikuta akichezea kichapo kwa madai ya kunaswa na mke wa mtu kisha kutembezwa mtupu mtaani.



Fumanizi hilo lililojaza umati wa jinsi na rika zote wakiwemo watoto lilijiri katikati ya wiki hii, maeneo ya Mji Mpya ndani ya chumba na kitanda cha wanandoa hao.

Kwa  mujibu wa majirani, jamaa huyo anadaiwa kuwa na kasumba ya kumhonga vyakula mke huyo wa mtu ambaye naye kwa kukosa uaminifu kwenye ndoa alijikuta akiingia mkenge hasa mumewe anapokuwa safarini kwa kuwa ni mtu wa kusafiri katika biashara zake binafsi.

Ilidaiwa kwamba, mwanamke huyo hutumia mwanya huo kumwingiza mchepuko wake huyo kwenye chumba na kitanda anacholala na mumewe kisha ‘kufanya yao’.

Baada ya kukolea huku mahaba niue yakitajwa na sauti ‘tamutamu’ zikisikika chumbani, majirani walikerwa na kitendo hicho cha jirani yao kudhulumiwa ‘mali’ zake ndipo wakaamua kumpa  taarifa mumewe.

Ilisemekana kwamba, mume, akishirikiana na majirani aliowaomba ushirikiano, aliweka mtego ambapo alijifanya anasafiri kama kawaida.


Siku ya tukio, saa husika ilifika, kama kawaida jamaa alifika nyumbani kwa wanandoa hao kisha kuchoma chumbani kwa wanandoa tayari kwa kulicheza ‘segere’.

Mwenye mke, akiwa chimbo alitonywa na majirani kuwa mambo ‘yamekwiva’ chumbani ndipo akawaibukia na kumkuta jamaa laivu akiwa mtupu. Haikujulikana kama ilikuwa ‘tayari au bado’.

Akiwa na hasira, mwenye mke alidaiwa kumshushia kipigo mgoni kilichomfanya kuloa damu chapachapa na baadaye kumtoa nje akiwa mtupu kisha kumtembeza mtaani kwenda nyumbani kwake huku ‘kadamnasi’ ikipiga kelele ‘watu weweee...”

Katika hali ya kushangaza, mwenye mke aliomba mkewe asipigwe picha akidai bado anampenda na hayuko tayari kumuacha.

Credit: Gpl/Risasi
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad