Ney wa Mitego na Jack Wolper Kuibua Mahusiano ya Kimapenzi Upya

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Na Musa Mateja
BAADA ya kudaiwa kuwa wapenzi na kisha habari hizo kufifia, hatimaye penzi la mwigizaji wa filamu za Kibongo, Jacqueline Wolper na Mbongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’, limeibuka upya ambapo safari hii Nay ameamua kufunguka hadharani.

Kwa mujibu wa chanzo makini,  wawili hao walianzisha uhusiano wao mwishoni mwa mwaka jana na sasa mapenzi ndiyo yamekolea hadi kufikia hatua ya Nay wa Mitego  kuanika hisia zake mtandaoni.
“Wamekuwa wakibanjuka kwa siri sana si unajua Nay ana mchumba wake Siwema, bado hajafanya maamuzi magumu ya kumtosa,” kilisema chanzo chetu.

Paparazi wetu alifanikiwa kunasa ujumbe wa Nay wa Mitego  kwenye mtandao wa Instagram ambao ulionyesha wakiitana kwa majina ya wapendanao kuonesha dhahiri wawili hao ni wapenzi.
Mbali na kuitana huko, Nay alionesha kuwa amemmisi Wolper ambapo muda mchache baadaye naye alijibu kwa kuwa amemmisi pia  kisha Nay akaifuta posti hiyo baada ya kuandamwa na maneno ya wapambe.

lipoulizwa Wolper kama kwa sasa ameamua kutulia na Nay wa Mitego na mipango ya uhusiano wao ipoje,  alikataa kufunguka moja kwa moja.“Kiukweli Nay ni mshikaji wangu tu, unajua nini? Kwa sasa siko tayari tena kumwanika bwana au mchumba wangu kama nilivyofanya mwanzo kwa Dallas, nitakuja kumweka wazi labda mwanaume nitakayezaa naye au atakayenioa kabisa,” alisema Wolper.

Kwa upande wake Nay alipoulizwa kuhusu uhusiano wake na Wolper na hatua ya kuunadi uhusiano wao mtandaoni huku ikifahamika kuwa ana mchumba mwingine, hakutaka kufafanua zaidi ya kujibu:

“Mimi huwa siangalii nani atasema nini wala atafikiria nini, mimi nilimmisi Wolper wangu, sikuwa na namna zaidi ya kutumia peji yangu kama nilivyofanya, tena siku hiyo alikuwa hapatikani hewani nikaamua kumtupia mtandaoni bila hofu kwani ni mtu wangu wa karibu na siogopi kitu juu yake,” alisema Nay wa Mitego.
GPL
---------------------------

Keep looking up! I learn from the past, dream about the future and look up. There's nothing like a beautiful sunset to end a healthy day.

----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad