Polisi wa Pikipiki Waporwa Bunduki 2 kwa Kushikiwa Kisu na Kujeruhiwa

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Watu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi, wamewavamia na kuwajeruhi askari mwenye no G369 PC Mansour na Hv507 PC Mwalimu, wakiwa doria ya pikipiki ambao walinyang'anywa silaha mbili aina ya SMG no 14301230 na 14303545 na watu wasio julikana mkoani Tanga.

Taarifa ya Jeshi hilo kwa vyombo vya habari imesema tukio hilo limetokea Januari 26, 2015 majira ya saa 23:30hrs eneo la barabara 04 jijini humo.

Aidha, imesema mmoja wa majeuhi askari mmoja no H 507 PC Mansour amejeruhiwa vibaya maeneo mbalimbali ya mwili na amelazwa katika Hospitali ya Mkoa Bombo.

Katika uchunguzi wa awali Polisi wamefanikiwa kumtia hatia hatiani mtuhumiwa mmoja, Ayubu Haule, (27), fundi Radio Mkazi waCorner Z Amboni Kiomoni ambaye alikamatwa eneo la tukio akijaribu kutoroka na pikipiki na mara baada ya kupekuliwa ndipo alipokutwa na mchoro wa ramani unaoonyesha matokeo ya Barabara na kufunguliwa kesi yenye no TAN/IR/322/2015.

Mtuhumiwa anaendelea kuhojiwa na Jeshi hilo huku timu ya Intel na makachero wa Polisi ikiendelea kufanya doria pamoja na Section 2 za FFU.

Picha za tukio:
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Tanzania inanuka sasa,yaani hata polisi hawaogopwi jamani!

    ReplyDelete
  2. Aiseee sijui Nchi inaelekea wapi!! Kweli usalama wa Raia upo kweli?? Nadhani kila mtu inabidi awe jambazi kha!!

    ReplyDelete
  3. mi nadhani mafunzo yatolewe kikamilifu wa napokua mafunzoni

    ReplyDelete
  4. Hapa tulipofika ni matokeo ya ubinafsi uliokithili wa viongozi. Wanajiona wana hati miliki ya kufanya kila kitu wao. Kundi kubwa la vijana waliokata tamaa limeachwa halina hata pa kushika. AJIRA, BIASHARA, MIKOPO, SCHOLARSHIP, PROJECTS hadi BIASHARA ZA UNGA vimehodhiwa na wakubwa pamoja na familia zao. Viongozi watafakari na kuchukua hatua, hatujawahi kushuhudia haya. POLENI SANA VIJANA WETU

    ReplyDelete

Top Post Ad