Walio Naswa Wakifanya Mapenzi ya Jinsia Moja Kumbe Walikuwa Wameoana Kabisa

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Na Haruni Sanchawa/Uwazi
SAKATA la wasichana wawili warembo, Maua Sadick (24) mkazi wa Stakishari, Ukonga, Dar es Salaam na Lucy Fred (23) mkazi wa Karakata, Dar ambao walishikiliwa katika Kituo cha Polisi Stakishari, Ukonga jijini kwa madai ya kufanya mapenzi ya jinsia moja limechukua sura mpya.

Habari za kipolisi zinasema wasichana hao ambao walifunguliwa jalada kituoni hapo namba SKT/RB/463/2015 baada ya kukamatwa Januari 12, mwaka huu inadaiwa kuwa walioana.

“Zipo picha zinazodaiwa kuwa walioana na wanaonekana wakiwa wanavishana pete nyingine wakiwa wanafungua shampeni kwenye hafla fupi ambayo waliifanya jijini Dar es Salaam,” kilisema chanzo ndani ya jeshi la polisi.

Habari zaidi zinadai kuwa hafla hiyo waliifanyia katika ukumbi mmoja (jina tunalihifadhi) ambao upo Chang’ombe na unatumika kwa shughuli nyingi za burudani na hata michezo.“Mimi nilihudhuria sherehe hiyo na picha ninazo ambazo zinawaonesha wasichana hao wakivishana pete na walikuwepo pia waalikwa kama unavyoona kwenye sherehe za harusi katika jamii yetu,” alisema mtu mmoja ambaye jina lake tunalihifadhi.

Mtu huyo alidai kuwa mmoja wa wasichana hao anamfahamu kwa kuwa sasa hivi anaishi kwa dada yake karibu na Uwanja wa Ndege, Karakata nyuma ya msikiti mpya.Mara baada ya kukamatwa wasichana hao, Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mogo, Stakishari,George Mtambalike alilithibitishia gazeti hili ofisini kwake kutiwa mbaroni kwao kwa madai ya kufanya mapenzi ya jinsia moja.

Naye Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi Ilala, SACP Mary Nzuki alisema wasichana hao bado wanapelelezwa. “Ni kwamba kesi yao ipo Stakishari na uchunguzi dhidi yao ukikamilika watafikishwa mahakamani, “ alisema Kamanda Nzuki.
GPL
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kwa hivyo..si,uache wafanye wanavyotaka....yawahusu nini nyie....mbona ulaya kitu cha kawaida..washamba nyie

    ReplyDelete
    Replies
    1. Huko ni ulaya usifananishe na huku sheria hairusu, acha umburura wewe.

      Delete
  2. hata vitabu vyadini vinakaza unae wasapoti labda na wewe umeolewa

    ReplyDelete
  3. Mdau juu ulaya wanafanya ksbb hawamjui mungu wala hakuna hoja yoyote uliotoa ya maana zaidi ya kuonyesha kuwa huna uwazo wa kutafakali bali kuinga kutoka kwa ur slave master, ukiunganisha asi na chanya unapata nguvu(mwanga) uke na um e unapata mtoto sasa wewe uambie ulimwengu faida yao madada? Wazazi wao wangefuata huo ulaya wako wenyewe wengezaliwa? Nadhani umeona wewe ndio mshamba lol

    ReplyDelete
  4. Ulaya uaya kunani ulaya kijana hapo juu? MUNGU ameumba jinsi mbili tofauty ili kuridhishana kimapenzi,kwanza kosa kwa MUNGU na kwa MUNGU hakuna khiary,watu wa LUTY walifudikizwa kwa dhambi ya kufanya mapenzi ya jinsia moja,pii sisi wa Africa pia ni kinyume na utamaduni wetu,SERIKALI iwachukulie hatua kali ili iwe fundisho kwa wengine wenye mchezo km huo...

    ReplyDelete

Top Post Ad