Watoto Wanne wa Familia Moja Wafariki Kwa Sumu Iliyowekwa Kwenye Chakula, Baba yao Anusurika

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Watoto wanne wa familia moja wakazi wa kijiji cha kibambila wilayani Kakonko mkoani Kigoma wamefariki dunia na mmoja amelazwa katika kituo cha afya Kakonko baada ya kula chakula kinachosadikiwa kuwa na sumu.

Makaburi yakiandaliwa kwa ajili ya maziko ya watoto hao

Mganga  mkuu wa wilaya ya Kakonko  Dkt. Fadhil Seleman  amewataja watoto hao waliofikishwa kituo cha  afya  Kakonko kuwa ni  Neema Joseph, Jonas Joseph, Majaliwa Joseph, Yusuph Joseph wote wakiwa na umri wa kati ya miaka 11 na 18 walifikishwa hospitalini hapo  wakiwa na hali mbaya na walipoteza maisha wakati wanaendelea kupatiwa huduma.
Amesema kwamba uchunguzi wa awali umeonesha kuwa watu hao wamekula sumu katika chakula cha ugali.

Akizungumzia tukio hilo baba wa watoto hao Joseph Kajolo ambaye alinusurika katika tukio hilo amesema hajui chanzo cha tukio hilo huku baadhi ya wananchi wa Kakonko  wameeleza kusikitishwa kwao na tukio hilo na kwamba vifo vya sumu katika wilaya hiyo  vimekuwa vikijirudia mara kwa mara

 Mkuu wa wilaya ya Kakonko Peter Toyima amesema polisi inamshikilia mtu mmoja kuhusiana na tukio hilo huku akiwataka wananchi kuacha vitendo vya kuwekeana sumu…
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. JAMANI WATANZANIA KWA NINI TUNAUANA VIBAYA HIVI JAMANI. EEE MUNGU WETU TUEPUSHE NA BALAA HILI LA KUUWANA. SASA NYIE MLIOUA HAO WATOTO MMEPATA FAIDA GANI???

    ReplyDelete
  2. sheria ichukue mkondo wake kuwa baini walio tenda maovu hayo

    ReplyDelete

Top Post Ad