'HAKUNA MASKINI JEURI.. Na Ukiwa Maskini Jeuri Utakuwa Maskini Milele' Zamaradi Afunguka

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


HUTAKIWI KUWA NA HASIRA KATIKA PROCESS ZA KUTAFUTA MAISHA.... utakutana na changamoto nyingi sana na lazima ukubali.. kubali kudharauliwa, kubali kushushwa kubali kuonekana huna maana lakini lengo ni ufikie pale ambapo siku moja kila mtu atakuheshimu..

Lakini ukianza kuchukulia kila kitu personal, kuwa na vinyongo na watu na kukataa dharau za huku chini trust me HUTOFIKA POPOTE.. Ukitaka kuvimba kabla hujafika utachelewa.. wenye mivimbo wengi hawajafika mbali kwenye maisha.. kumbuka tu BOSS HANUNIWI!!! Huu msemo una maana kubwa sana pamoja na kwamba kila mtu anautafsiri kivyake.. lakini ni sawa na kusema tumikia kafiri upate mradi wako.. unachokihitaji wewe unakijua..

DHARAU zake ama chochote chake fanya kama hazikushughulishi.. maisha ni safari ndefu na hakuna aliewahi kuahidi kwamba itakuwa ni safari rahisi.. kubali vikwazo kama sehemu ya safari.. na wengi waliojishusha katika kutafuta tumeona matunda yao asikudanganye mtu HAKUNA MASKINI JEURI.. Na ukiwa maskini jeuri utakuwa maskini milele... ndivyo ilivyo na SI kwamba ni kitu kizuri ama kinasapotiwa.. la hasha!! Ila ndivyo maisha yalivyo.. wanasema LIFE IS NOT FAIR!!

 Haikugharimu kuwa mpumbavu pale ambapo unaona kuna faida na wewe.. unachotakiwa kujua 'KUJIFANYA MPUMBAVU mbele ya mtu ANAEJIONA MWEREVU ni kumfanya YEYE mpumbavu bila kujua...' kumbuka tu usije ukatumia hii vibaya ukajikuta umekuwa MPAMBE badala ya mtu anaetaka kutimiza ndoto zake - Zamaradi.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

9 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. kweli mtupu zama, bora Wema akae kimya na afanye yake. awaache wauza sura.

    ReplyDelete
    Replies
    1. We naeeeee!!! Kichwa chako unakitikisa maji tu yamejaaa unamuwaza wema tuuu mwili mzima umemchora wema tuu unaonekana unaitaji msaada mkubwa sana wa kisaikolojia pole weeee!!!

      Delete
    2. Daaaa yani zama umeongea maneno yako hayo yamenitia moyo sana yani nimekupenda bure zama kumbe unajua kumpa mtu moyo hivyoo!! Nakumbuka nilishawahi kupitia situation kama hiyo watu walikuwa wananiona mie mjingaaaaa lkn kwa kuwa nilijua ni nini natafuta maishani nilijishusha na neno samahani kwa boss sikuacha pale nilipo kosea aisee nashukuru mungu sana hapa nilipo fika.

      Delete
  2. Mweeee zamaradi maneno yako yamenigusa sanaa. Yamenipa nguvu ya kusonga mbele zaidi kweli kabisa boss hanuniwi jamani!!!

    ReplyDelete
  3. yesss zama ndo maana Wema kaa kimya kumbe anaakili kama wewe.

    ReplyDelete
  4. umeongea bibie big respect siku zote nakuona uko juu asante kwa maneno mazito 2015 naongeza nguvu

    ReplyDelete
  5. Dah maisha kweli usikate tamaa zamaradi umetoka mbali sana nakukumbuka wakati umehamia cambridge na sasa hivi

    ReplyDelete
  6. Ni maneno 2 zamaradi ambayo watu huamua kujiita kweli hakuna masaskn jeuri

    ReplyDelete

Top Post Ad