JB, Mzee Majuto na Richie Wamtembelea Mama wa Mtoto Albino Aliyeuawa…Wamwaga Machozi

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Wikiendi iliyopita staa wa sinema za Kibongo, Jacob Steven ‘JB’ alijikuta akiangua kilio na kuungwa mkono na mastaa wenzake, Amri Athumani ‘Mzee Majuto’ na Single Mtambalike ‘Richie’ walipomtembelea wodini mama mzazi wa mtoto Albino, Yohana Bahati (1) aliyeuawa kikatili, Ester Thomas (30) ambaye naye alijeruhiwa vibaya kichwani, Ijumaa Wikienda linakuhabarisha.

Tukio hilo la majonzi lilijiri kwenye Hospitali ya Bugando mkoani hapa ambapo wasanii hao walikwenda kumfariji mama wa mtoto huyo aliyetekwa mjini Geita hivi karibuni.

Walipofika wodini hapo, JB na wenzake walitoa yao ya moyoni kupinga vikali ukatili aliotendewa mama huyo na mwanaye huku wakitahadharisha juu ya laana inayoweza kuikumba jamii yetu kwa tukio hilo.

JB: Nampa pole sana mama Yohana. Hii ni aibu kubwa kwa taifa letu na jamii pana duniani.
Watu hawafanyi kazi kujipatia kipato halali. Mafisadi wanataka kujipatia fedha kupitia njia za kishetani za kuwaua wenzetu. Albino ni wenzetu na tunawapenda. Lazima wahalifu wakamatwe na wahukumiwe kunyongwa.

Mzee Majuto: Inasikitisha sana. Haivumiliki. Albino ni wenzetu na wana uwezo mkubwa wa kulisaidia taifa letu. Wahusila lazima wakamatwe na tuone wakichukuliwa hatua kali.
Richie: Natokwa na machozi. Hiki ni nini? Hatuwezi kufumbia macho jambo hili hasa sisi wenye nafasi kubwa ya kukemea vitendo hivi.

Mara baada ya mastaa hao kutoa la moyoni katika wodi aliyolazwa mama huyo, iligeuka kama msiba kwani kila aliyekuwepo alikuwa akiangua kilio kwa uchungu.

Tayari mtoto Bahati amezikwa baada ya mwili wake kupatikana ukiwa hauna baadhi ya viungo huku mama yake akiendelea na matibabu baada ya kufanyiwa oparesheni sehemu ya kichwani aliyojeruhiwa vibaya wakati akinyang’anywa mwanaye.

Tunampa pole sana mama Yohana Bahati, watanzania tuungane kupinga ukatili huu.

GPL
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

6 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. wote waliohusika na kitendo hicho cha kikatili na walaaniwe na mungu wa mbinguni na wasifanikiwe katika jambo lolote.

    ReplyDelete
  2. Watanzania hata tutoe machozi leo sina UHAKIKA MUNGU hatatuona tu WANAFIKI WAKUBWA inasikitisha WAZIRI MKUU alipata kutoa MACHOZI akatamka kuwa HAWA WAUAJI WANAPASWA KUUAWA bunge na wabunge wakashikilia bango kuwaWAZIRI MKUU kahalalisha MAUAJI na hawalilii ALBINO ila analilia UWAZIRI MKUU kwa kuwa walijadili hadharani TVzikionesha ni vema waliomkashfu waziri mkuu wawekwe hadharani hawa ni wauaji namba moja kwani ndio waliohalalisha MAAUJI tuache unafiki huu ni uvunjaji wa haki za binadamu iwapo hao ndio watunzi wa sheria wanabariki mauaji kuna haja gani waendelee kurudi bungeni kwenye kesi ya uvunjifu wa haki za binadamu ICC hawa ni mashahidi namba moja naomba umoja wa mataifa usiishie kulaani hatua kali zichukuliwe .SERIKALI,BUNGE,MAHAKAMA ,NA WATETEZI WA HAKI ZA BINADAMU TANZANIA hawapaswi kuzungumzia lolote kwani sio tukio jipya ALBINO WAPEWE FURSA YA KUTEUA WATETEZI WAO

    ReplyDelete
  3. Inaskitisha na kufedhehesha sana huna budi kuzuia machozi yako.

    ReplyDelete
  4. Aloo hii inatisha sana, yaani tumekua kama tuko porini vile, yaani kama wanyama loo m/Mungu fanya lolote, angamiza vizazi vyote vilivyopo, na ulete vinavyokuogopa na kukutii!. Ee maana tumeshindwa kusaidia wenzetu , waende wapi sasaaaa AAA.

    ReplyDelete
  5. WATANZANIA TUUNGANE KUUKEMEA UKATILI HUU ULIOPITILIZA!!!

    ReplyDelete
  6. Serikali iwajengee kituo Chao na ulinzi mkali ndio dawa

    ReplyDelete

Top Post Ad