Kiukweli Wanigeria Hawatuwezi Kimuziki-Ben Pol

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Msanii Ben Pol ambae kwa sasa anafanya poa na kazi yake mpya ya Sophia amefunguka na kusema kuwa wasanii wa Nigeria hawawawezi wasanii wa bongo kwa kipaji na kutengeneza ngoma kali na hilo amelithibitisha msanii Diamond Platnum ambae kwa sasa anafanya poa na wimbo wake wa Nitampata wapi ambao unaoneka kufanya vizuri zaidi kuliko hata ngoma za wasanii wa Nigeria katika baadhi ya vituo vya habari ndani na nje ya Tanzania.

Ben Pol amesema hayo kupitia Account yake ya Twitter ambapo amesema msanii Diamond kishamfunga paka kengele na kilichobaki ni kuongeza nguvu na kuona ni jinsi gani wanaweza kupenya zaidi na kuzidi kutanua mipaka ya Bongo fleva ulimwenguni.
"Kiukweli Wanigeria Hawatuwezi Kimuziki,Na kuhusu Nani Atamfunga Paka kengele, Tayari Diamond Ameshamfunga Paka kengele"
Ben Pol amekuwa msaniii wa pili kuonyesha kuwa muziki wa Bongo fleva ni muziki mzuri kuliko muziki wa Nigeria kwani hata msanii Mwanafalsafa alishasema kuwa haupendi na haukubali kabisaa muziki wa Nigeria.Licha ya baadhi ya wasanii kuusujudu na kuamini ndiyo muziki mzuri na ambao wanahisi unapendwa sana kwa sasa lakini kwa Mwana Fa imekuwa tofauti kwani alisema "Katika Habari nyingine,nimeamua kuwa hater wa mziki wa Nigeria".
Kwa upande wake Diamond amezidi kushukuru Mungu kuona wimbo wake huo wa Nitampata wapi unazdi kuchana mawimbi na kupokelewa vizuri hata nje ya Afrika Mashariki kitu ambacho kinamfanya kujiona ni balozi mzuri zaidi wa Afrika Mashariki.
"Asante Sana Mwenyez Mungu kwa Baraka zako zinazonifanya nizidi kuiwakilisha vyema Nchi yangu na Afrika Mashariki yangu..."
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. ...pumbafu sana wewe, domo kama samaki..ndiyo maana hamfiki mbali mumeridhika na ujinga..eti wanigeria hawatuwezi kimuziki... kwa muziki gani? huo wa kubana pua.. muziki wa ku-copy na ku-paste pasipo stahili, muziki ambao hamuwezi hata ku-perform live... mnajitahidi ndiyo, lakini kuwafikia na kuwapita wanigeria bado saana..vuta soksi na siyo kujisifia ujinga

    ReplyDelete
  2. Yeah right ben!! Wenzenu wanaimba kizungu ndo maana wamewaacha english ni universal language,ndio mna kipaji sana lakini ndo hivyo,angalia my number one ya diamond davido kampaaisha chibu sababu jamaa ndo wameshika africa,badilikeni na wakati

    ReplyDelete

Top Post Ad