Mwanamke Auawa na Mumewe Kwa Kipigo na kisha Mwili wake Kufukiwa katika Zizi la Ng'ombe

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mwanamke mmoja mkazi wa Kijiji cha Ubetu Wilaya ya Rombo mkoani Kilimanjaro, amefariki dunia baada ya kupigwa na mume wake sehemu mbalimbali za mwili na kisha kuzika mwili wake kwenye boma la ng'ombe.

Kamanda wa Polisi mkoani Kilimanjaro, Geofrey Kamwela, alisema tukio hilo lilitokea Februari 25 mwaka huu saa 11:45 jioni.
 
Akieleza mazingira ya tukio hilo, Kamanda Kamwela, alisema siku ya tukio jirani na familia hiyo alipigiwa simu na mume wa marehemu na kumwambia ameuwa mkewe na kumtelekeza ndani ya bomala ng’ombe.

Kwa mujibu wa kamanda, mwanamke huyo aliyeuawa ametajwa kuwa ni Jenipher Peter (45). Alisema alikuwa akiishi na mume wake, Peter Mrosso (43) pamoja na watoto wao watatu. Alisema mwili wake ulifukiwa ndani ya boma la ng'ombe.

Kamanda alisema taarifa za mauaji ya mwanamke huyo ilitolewa baada ya jirani yake kupigiwa simu na mume wa marehemu, akimtaarifu kuwa amemuua mkewe na maiti ameifukia ndani ya boma la mifugo.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Eeeh Mungu,yaani hii dunia kila siku inakuwa kama jana,yaani watu wanakemea vitendo viovu lakini ndio kwanza watu wanaendeleza.Mbaya zaidi huyu kakiri kufanya mauaji mwenyewe,lakini si ajabu tukamuona mitaani baada ya muda si mrefu.

    ReplyDelete
  2. huyu baba kachanganyikiwa kama siyo kuwehuka kabisa. inaonekana hakukusudia kuuwa.

    ReplyDelete
  3. nilijua mambo hayo ni kanda ya ziwa peke yake hadi kilimanjaro duuu majanga

    ReplyDelete
  4. Wameishi miaka mingi wamejaliwa watoto 3 huyo jamaa sio chizi kuna sababu iliyompelekea kufanya hivyo tusilaumu tu moja kwa moja hawa kina mama wakati mwingine wanakuwa kama kaa la moto

    ReplyDelete

Top Post Ad