Skendo ! Lulu na Wolper Waonyeshana JEURI ya Mabwana

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Sakata la kupangishiwa nyumba za kifahari na wanaume linazidi kuchukua sura mpya kwa mastaa wa kike ndani ya tasnia ya sinema za Kibongo ambapo safari hii mastaa wawili, Elizabeth Michael ‘Lulu’ na Jacqueline Walper ‘ Wolper’ Massawe wanadaiwa kuoneshana jeuri ya mabwana wakipima ni yupi mwenye mshiko zaidi huku akina Wema Isaac Sepetu na Kajala Masanja ambao awali walikuwa juu wakipotezwa.

TAMBO ZA NANI ZAIDI?
Uchunguzi wa Ijumaa umebaini kwamba, kumekuwa na kasumba ya baadhi ya mastaa hao kutambiana kuwa ni nani zaidi anayemiliki bwana mwenye mawe au mshiko kuliko wengine.

Ilidaiwa kwamba, baada ya Lulu kuripotiwa kupangishiwa bonge la jumba la kifahari na milionea maarufu wa jijini Arusha lililopo maeneo ya Mbezi-Beach jijini Dar, Wolper naye anadaiwa kujibu mapigo kwa kupangishiwa mjengo wa maana na bwana’ke uliopo maeneo hayohayo.
Kwa mujibu wa vyanzo vyetu ambavyo ni watu wa karibu wa mastaa hao, kwa sasa wawili hao ni moto wa kuotea mbali kwani kila mmoja amepata bwana mwenye ‘mpunga’ mrefu.

WOTE WANALIPA SH. MIL. 30
Ilidaiwa kwamba, kama ilivyokuwa kwa Lulu, Wolper naye analipiwa nyumba hiyo kiasi cha dola za Kimarekani 1,500 kwa mwezi (zaidi ya Sh. milioni 2.4) karibia Sh. milioni 30 kwa mwaka.

CHUMBA KAMA BOUTIQUE
Habari zilidai kwamba, kama ilivyo ya Lulu, nyumba hiyo aliyopangishiwa Wolper ina vyumba kibao vya kulala, ukumbi wa wageni, sehemu ya kulia chakula, mabafu, majiko n.k.
Pia nje ya nyumba hiyo kuna eneo kubwa la bustani iliyopambwa kwa maua mazuri na eneo la kutosha la maegesho ya magari.

Pamoja na kupangishiwa mijengo hiyo ya kifahari ushuani, Lulu na Wolper wamekuwa wakioneshana jeuri ya magari waliyonunuliwa na mabilionea hao.

MAGARI
Uchunguzi unaonesha kuwa Lulu ana mkoko aina ya Toyota Rav4 New Model wenye thamani ya zaidi ya Sh. milioni 30.Kwa upande wake Wolper anasukuma ndinga aina ya Toyota Prado, nalo lina thamani ya zaidi ya Sh. milioni 30.

WATOFAUTIANA VITU VICHACHE
Habari za ‘kiubuyu’ zinadai kwamba wawili hao wanapishana vitu vichache mno kama vile aina ya mawigi na aina ya maisha (life style) ambapo bwana wa Wolper amempiga ‘stop’ kuigiza lakini bado Lulu anapiga mzigo.

“Lulu na Wolper wamelamba bingo za nguvu na bahati nzuri wanaonekana wote kupata mabwana wasiokuwa na sifa.“Kwa mfano, Lulu pamoja na kuishi katika maisha mazuri bado anasomeshwa na tayari ameshakamilishiwa ujenzi wa nyumba yake ambayo juzikati alimkabidhi mama yake kama zawadi.

WOLPER AKOSWA, MAJIRANI WAFUNGUKA
Ijumaa lilimtafuta Wolper kupitia simu yake ya mkononi lakini iliita bila kupokelewa. Mwandishi wetu alifika mtaa anaoishi Wolper, akagonga sana geti lakini halikufunguliwa.Hata hivyo, majirani wa staa huyo wamedai kuwa amekuwa akionekana akiingia na kutoka akiwa ndani ya gari hilo aina ya Toyota Prado. Jitihada za kumtafuta zinaendelea.

----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

6 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. hii sio habari ya kutuandikia badala muhamasishe watu wapige mzigo wapate hela zao mnawapa sifa za kijinga eti mabwana kweliiiiiiiiiiii?upumbavu mtupu huu

    ReplyDelete
  2. Acheni usenge na sifa za kipumbavu, mnaacha kusifia na kuwahimiza kujituma katika kazi eti mabwana hovyoooo

    ReplyDelete
  3. MIYE NADHANI WANAONYESHA JEURI NYUMBA ZAO KUMBE ZA KUPANGA!!!! UJINGA MTUPU!!

    ReplyDelete
  4. Sijawahi kuona mtu anaandika ujinga kiasi hiki mpaka mimi msomaji najiona mjinga hata nilivyosoma, mjipange hizi sio habari angalau mngeandika wanashindana kununua viwanja? Habari hii inafundisha nini jamii zaidi ya kuongeza maambukizi ya ukimwi? Mjipange sio kila habari ni habari lazima iwe na maudhui ya maana

    ReplyDelete

Top Post Ad