Wimbi la Kumshawishi Edward Lowassa Kugombea Urais Lazidi Kupamba Moto.

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Wimbi la watu kumuunga mkono na kumshawishi Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa, kugombea nafasi ya urais wakati utakapofika, limezidi kupamba moto na safari hii, ujumbe mzito kutoka Pemba unajiandaa kufanya hivyo.

Taarifa za maandalizi kwa wananchi na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutoka Pemba kwenda Monduli kumshawishi Lowassa kugombea urais, zimekuja siku chache baada ya baadhi ya wananchi na wanachama wa CCM Kanda ya Ziwa, kufanya hivyo wiki iliyopita.

Wananchi hao katika kutimiza dhamira yao, walimtuma Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya chama hicho taifa, Dk. Raphael Chegeni, kwenda kumshawishi Lowassa ili awanie nafasi hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari Monduli jana,  Mjumbe wa Halmashauri ya chama hicho taifa, (NEC) kutoka Wilaya ya Chake Chake Pemba, Daud Ismali, alisema amekwenda Monduli kumshawishi Lowassa kugombea nafasi ya urais muda utakapofika.

Ismail ambaye ni mdogo wa Makamu wa Rais, marehemu, Dk. Omar Ally Juma, alisema kwenda kwake Monduli ni kufanya maandalizi ya ujumbe mzito utakao toka Pemba kwenda kumshawishi agombee urais.

“Watakuja kumwomba mheshimiwa Lowassa kugombea urais, uamuzi wa kugombea au kutogombea ni wake."

Akieleza kwanini waje kumshawishi Lowassa badala ya mtu mwingine, alisema ni kutokana na utendaji na uadilifu wake.

Pia alisema, “jina la mheshimiwa ni kubwa na siyo Pemba tu hata ukienda Marekani ukiuliza ni jina gani linazungumzwa kuhusu urais utaambiwa ni Lowassa.

“Ukienda mtaani kukusanya data za aina yoyote ile, jina linalotajwa kuwa linafaa kuwania nafasi hiyo ni la Lowassa,” alisema.
Mpekuzi blog
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad