Diamond na Penny Katika Mzozo Mpya..Yadaiwa Penny Alidanganya Kuwa Ana Mimba ya Diamond

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mtangazaji wa Efm Radio, Penieli Mungilwa ‘Penny’ akiwa na aliyekuwa mpenzi wake Nasibu Abdul ‘Diamond’.
IMEVUJA! Ile mimba ya aliyekuwa Mtangazaji wa Efm Radio, Penieli Mungilwa ‘Penny’ ambayo ilijulikana alipachikwa na staa wa muziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ imezua mzozo upya baada ya kuvuja kwa madai mengine.

Chanzo makini kimeliambia Amani kwamba, tofauti na madai ya Diamond kwamba Penny alitoa mimba yake, lakini kumbe Diamond hakumpa mimba ila ilikuwa ni magumashi ya Penny.

SIKIA HII
“Hali ilikuwa hivi! Kutokana na Diamond kutafuta mtoto kwa muda mrefu, hasa kwa mpenzi wake wa nyuma Wema Sepetu kushindikana, ikabidi Penny atumie mbinu yake ili kufaidika na pesa za Diamond.
“Penny aliahidiwa na Diamond kwamba, kama atakubali kuzaa naye atamnunulia gari zuri, kwa hiyo kazi ikawa kwa Penny sasa, afanyaje?

“Siku moja Penny alimwambia Diamond kwamba amenasa, Diamond akafurahi sana, lakini kumbe Penny alishaenda kwenye hospitali moja kubwa iliyopo Kinondoni (jina tunalo), akaongea na nesi mmoja kwamba kama atakwenda na Diamond kupima mimba akubali kwamba anayo, lengo lake ni kupata gari,” kilisema chanzo hicho.


IKAZIDI KUDAIWA
Chanzo kikazidi kudai kwamba, ili amridhishe Diamond, Penny alimchukua mpenzi wake huyo hadi kwenye hospitali hiyo na kukutana na yule nesi ambaye alimwambia Diamond kwamba kweli mchumba wake huyo (kwa wakati ule) alikuwa amenasa.“Ndipo Diamond ikabidi amnunulie gari Penny aina ya Toyota Brevs la rangi ya bluu iliyoiva. Siku mbili tatu, akageuka, akamwambia Diamond mimba imetoka, ndiyo kikawa kisa cha kumwagana,” kiliongeza chanzo chetu.

PENNY ASAKWA NA AMANI
Baada ya kupata madai hayo mazito, Amani lilimvutia ‘waya’  Penny  na kumsomea mashtaka yake ambapo alisema kuwa, hafikirii katika kumbukumbu zake kama alishawahi kusema yeye ni mjamzito au alikuwa na mimba ya Diamond kama siyo mwanamuziki huyo kutangaza mwenyewe.

“Hivi jamani! Mimi sijawahi kusema kama nina mimba ya Diamond hata siku moja, sasa hapo hushangai aliyekuwa akisema nina mimba ni Diamond na siyo mimi. Kwanza Diamond hajawahi kunipa mimba hata siku moja, muulizeni aseme ukweli wake. Kama ni gari ni mapenzi yake lakini si zawadi ya mimba,” alisema Penny.


DIAMOND NAYE
Kwa upande wake, Diamond alipoulizwa kuhusu madai ya kuingizwa mjini na Penny kuhusu mimba, alikuwa na haya ya kusema:“Mm! Hiyo kali zaidi! Mimi Penny aliponiambia ana mimba yangu, asubuhi nilimkurupua mwenyewe, nikampeleka kwenye hospitali yangu mimi, hakunipeleka yeye.

“Tena hakujua kama nampeleka hospitali gani. Kule daktari wangu akampima, akamuona amenasa kweli. Sasa mnaposema eti alinipeleka kwenye hosptali yake aliyokwishapanga na nesi, nashangaa, siyo kweli bwana.“Yeye kama alifanya hivyo labda alimfanyia mtu mwingine, si mimi. Sasa naona kama kuna mzozo unataka kuibuka upya hapa.”

PENNY, ARUDIWA, HAPOKEI SIMU
Jumatatu iliyopita, Penny akapigiwa simu tena ili kupewa majibu ya Diamond, lakini simu yake iliita kwa muda mrefu bila kupokelewa. Lakini Amani linaendelea kumfuatilia ili kumsikia atasema nini kuhusu majibu ya Diamond.
~Globalpublishers
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Tafuta mambo yenyemaana yakuandika sie itatusaidia nini wakati hao watu wako ktk mahusiano mengine kwamuda mrefu nyie waandishi uchwara hamtaki kupanua mawazo kabisa kutwa Diamond / wema/masogange hebu kaeni muangalie mmeshawaandika mara ngapi tangu mwaka uanze ndio mtajua ujingawenu tumeshauchoka

    ReplyDelete
  2. JAMAN KWANINISIACHE YALIYOPITA. HUU NI UCHONGANISHI SI WAMESHAACHANA WAACHENI NA MAISHA YAO. HIVI WE MWANDISHI MBONA HABARI ZAKO NA MA EX WAKO HUZIWEKI GAZETINI KILA SIKU DIAMOND..TANZANIA NCHI YA AMANI ACHENI IZO.HAO NI WASANII WASIJESHINDWA KUFANYA KAZI PAMOJA.FUNIKENI JUNGU MWANAHARAMU APITE

    ReplyDelete
  3. OLD NEWS UDAKU HAMNA MPYA???????????????

    ReplyDelete
  4. shidaaaaa hiii mademu wasiku hizi pesa mbele!!

    ReplyDelete

Top Post Ad