MZEE YUSUPH: Nasikia Raha Sana Kuwa na Wake Wengi

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Unafahamu kama Mzee Yusuph anasikia raha kuwa na wake wengi, huku akihakikisha anawatimizia wote mahitaji yao? Fuatana nami ufahamu mengi zaidi kuhusiana na suala la ndoa kwa nguli huyo wa muziki wa taarabu hasa wenye vionjo vya mahaba.

Swali: Katika maisha yako umeoa mara ngapi?

Mzee Yusuph: Nimeoa mara tano, nilioa mke wa kwanza tukashindwana nikamuacha, wa pili nikamuacha, wa tatu pia nilimuacha lakini wa nne na wa tano nipo nao.

Swali: Kuna sababu kubwa ambayo unaamini mwanamke akiifanya, huwezi kuvumilia zaidi ya kumuacha?

Mzee Yusuph: Sina kosa maalumu, inapotokea mwanamke anakuwa mjuba nafahamu ameshachoka ninamuacha aende zake, lakini kukwambia kuwa hili ni kosa maalumu mwanamke akifanya namuacha sina.

Swali: Mke wa kwanza ulioa ukiwa na umri gani?

Mzee Yusuf: Naona una nichimba, sijui mpaka nikaangalie cheti changu cha ndoa ila nilioa Zanzibar.

Swali: Inasemekana kuwa unampenda sana Leyla kuliko mke mdogo Chiku. Je, hilo lina ukweli?

Mzee Yusuph: Halina ukweli wowote ndiyo maana nipo nao wote. Nakili kuwa kama binadamu huwezi kuwapenda wote sawa, lakini najitahidi kama tulivyoamrishwa na dini niwatimizie wote sawa na ndivyo ninavyofanya.

Mashallah! Katika kuwajali sawa najisifu mwanaume nimejipanga kuhakikisha hakuna anayenung’unika.

Sababu ya watu kusema nampenda sana Leyla kuliko bi mdogo ni kutokana na kuwa naye muda mwingi kwa sababu tunafanya kazi pamoja na kazi yetu inatukutanisha na watu wengi ambao hawauoni upande wa pili.

Ninapotoka na Chiku hawatajua kwa sababu hawatakuwa pamoja nasi. Na zipo safari nyingine nje ya kazi natoka na Leyla na hakuna anayefahamu pale wanapotuona mara nyingi tunakuwa kazini siyo matembezini.

Swali: Kuna tofauti gani ya kuwa  na mke mmoja au wengi?

Mzee Yusuph: Tofauti ipo kulingana na malengo ya muoaji, kuna wanaooa kwa mapenzi, kupata watoto wengi pia wapo wanaooa kwa ajili ya kukuza uchumi.

Hayo yote yameainishwa hata katika dini yetu ya Kiislamu, unaweza kumuoa mtu kwa ajili ya kumstiri labda alikuwa hapati mume. Vile vile unaweza kumuoa kwa kukuza kipato kwa sababu anaweza kuwa mchakarikaji mambo yakawa sawa nyumbani.

Lakini kwangu mimi ni mapenzi tu hakuna kingine, nimewaoa wake zangu kwa sababu nawapenda hayo mengine ni majaaliwa yanayokuja baada ya kuwaoa kwanza.

Wanaodhani kuoa wake wengi ni kwa ajili ya shughuli ya faragha pekee siyo kweli kuna vitu vingi vinatazamwa.

Asikuambie mtu kuwa na wake wengi kuna raha yake, unajidai, unajinasibu ukiwa nao wamekuzunguka, huku ukisikiliza manukato tofauti kutoka kwao na kila mmoja akikudekea anavyotaka na ukimudu kuwahudumia ndiyo raha zaidi, kama ambavyo mimi nafanya.

Swali: Kuna tabia ya wake wenza kutopatana, unakabiliana vipi na tatizo hilo?

Mzee Yusuph: Siyo tatizo ndiyo raha ya ndoa ya wake wawili, maana ukisema tatizo kwani lazima kuwa nao. Nakabiliana nalo kwa kuwa wote wangu najua jinsi ya kuwatuliza na wakanielewa.

Kizuri zaidi ninapokuwa nao hakuna anayeonyesha kukerwa na mwenzake wote wapo huru kuniambia chochote wanacheka na kufurahi, kama kuna hali tofauti wanapokuwa wawili hainishughulishi hadi niwaone ndiyo nitaliita tatizo maana watakuwa wameshanishinda.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

18 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kwakweli ukimwi hauishiiiiii,.. hv mfano una wake wanne upo zamu kwa mke mmoja hawa wengine wanakufayia zamu kisirisiri kwa michepuko yao,,. hv hapo kuna kupona kweli

    ReplyDelete
  2. kafiri ni kafiri tu hata comment zao zinajulisha tu kwa chuki. tumeruhusiwa kuoa wake 4 kwa mwenye kuweza kufanya uadilifu, takwimu ya ukimwi katika miji ambayo makafiri ni wengi ni kubwa kuliko miji ya kiislam,ajab kwa makafiri la kuruhusiwa kuoa mke zaidi ya mmoja inawauma, lakini wao wanaoa mmoja halafu ana vimada vingi huko mitaani na ndio maana ukimwi takimu yake ni kubwa katika miji yao,acheni michuki makafiri msi-comment kiushabiki na jazba za pombe na minguruwe na akili za propaganda.kufeni na chuki zenu.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kula 5 mdau! Mapadri hawaruhusiwi kuoa kabisa lakini, wanazaa hovyo na watawa wao (masister) pamoja na 'machangu'. Kuna padri ananyumba ndogo yake pande za magomeni kagera, anakuja usiku tu na anamuhudumia kila kitu, anamsomeshea watoto wake, misaada ya kanisani inaanzia kwake.......anatamani kumuoa huyo dada lakini sheria yao inambana.........poleni sana.

      Delete
    2. We Anonymous No. 2, umesema mmeruhusiwa kuoa wake 4, sasa hao wa Mzee Yusuph ni wa 4 si kazidisha, umekazana makafiri makafiri. Hao wote unaowasema hapo wamevunja sheria ya Mungu, Mungu aliumba mke mmoja na mume mmoja, alitoa mbavu moja akamtengenezea Adam mke, hivyo kuoa wake wengi ni dhambi maana si mpango wa Mungu. Pili hao wenye wake alafu wanakuwa na vimada pia ni dhambi kwa sababu na usiwaunganishe watu wote kwamba wanafanya hivyo wapo walio waaminifu kwa Mungu na wanatii maagizo ya Mungu ya kuwa na mke mmoja. Alafu kwa taarifa yako kafiri ni yule asiyetenda mapenzi ya Mungu na anayetukana kama wewe

      Delete
    3. We Anonymous No. 2, umesema mmeruhusiwa kuoa wake 4, sasa hao wa Mzee Yusuph ni wa 4 si kazidisha, umekazana makafiri makafiri. Hao wote unaowasema hapo wamevunja sheria ya Mungu, Mungu aliumba mke mmoja na mume mmoja, alitoa mbavu moja akamtengenezea Adam mke, hivyo kuoa wake wengi ni dhambi maana si mpango wa Mungu. Pili hao wenye wake alafu wanakuwa na vimada pia ni dhambi, usiwaunganishe watu wote kwamba wanafanya hivyo wapo walio waaminifu kwa Mungu na wanatii maagizo ya Mungu ya kuwa na mke mmoja. Alafu kwa taarifa yako kafiri ni yule asiyetenda mapenzi ya Mungu na anayetukana kama wewe

      Delete
    4. Hey nyie hapo juu mbona mmepanic sana Mweee poleni mkiambiwaga ukweli huwa mnalipuka kama moto wa kifuu!! Mtakomaaaaa kisonono, kaswende, pangusa nk.bora kuwa na mke mmoja mwaminifuu hata ukiwa na mchepuko kinga zipo sasa cjui we hapo wake wanne wachepuke cjui kama wanatumia kinga. Mnaloooooo.

      Delete
    5. kwanza neno kafiri nila mtu asiye mjua mungu wala asiye muabudu muumba waka pili jamani hakuna aliye mkamilifu mbele ya mungu isipokuwa yeye peke yake halafu awe padre awe shekhe wote ni wanadamu wana mapungufu yao kama wengine kama muislamu dini yake nikuoa wanawake 4 haya padre vimada haya hakuna atakaye kwenda kujibu mbele yake yeye yule aliyetuumba makosa ya mwenzie huo ndiyo mtizamo wangu

      Delete
  3. Kua na wake wengi ni Ujinga tu huo wewe mzee yusuf, watu wanajilia vyao kiuraiini pia utalea watoto si wako

    ReplyDelete
    Replies
    1. Nakupa like mdauu!! Kwanini usitulie na mmoja wapenda ngono haoooooo lkn hata wakristo wapo pia kama hao!

      Delete
  4. mshenzi mkubwa we unaetukana wakristo nyoko zako na mtakufa sana miaka hii mpaka umalaya uwaishe eti wake4

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mkristo mwenzangu umeniangusha!!! sasa mbona na wewe unatukana tena baada ya kumuambia kwa upole jamani.

      Delete
  5. MITARA INA FAIDA ZAKE MIMI NA WAKE WATATU SITOKI NJE YA NYUMBA WAKE WAWILI WOTE WAHASIBU NA MMOJA MFANYA BIASHARA MAISHA MAZURI NA TUNA KIPATO KIZURI SANA

    ReplyDelete
    Replies
    1. kwa taarifa yako unakula mavi na kula mikojo yao kama kawa kwani kila mke anafanya kitu ili umpende yeye zaidi ya wenzake kwa hiyo inaaminika mikojo na mavi inaua nguvu za uganga. kwa hiyo kila mtu anakuwa na bidii kuuwa uganga wa mwenzake kwa kukuwekea mavi au mkojo !! UPO HAPO????????

      Delete
  6. Ivi hamuezi kuandika kwa heshima wakristu wakristu tumewakosea nini kila mtu atabeba msalaba wake.

    ReplyDelete
  7. Mkristu Mkristu tumewakosea nini kila mtu naimani yake kila mtu atabeba msalaba wake lazima muwe wastarabu.

    ReplyDelete
  8. Ahaaaaaaaaa mke mmoja ndo mpangoooo

    ReplyDelete
  9. acheni mabishano. kuna waislamu mpaka wanakufa wana mke mmoja na wengine kama mzee yusuf kuna wakristo pia wana wake wengi na hata ndoa hawajafunga nao na pia wapo walio waaminifu na wana mke mmoja . kila mtu atabeba msalaba wake

    ReplyDelete
  10. huyo aliyeanza kutikana na hajui dunia inavyokwenda na hamuogopi Mungu ,Mungu akusamehe siku moja uje umjue yeye

    ReplyDelete

Top Post Ad