Ombi Hili la Wema Sepetu, Likufikiae na Wewe….Tubadilike

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

“Watanzania wenzangu, naombeni leo tujiulize: mitandao ya kijamii ina kazi gani kama sio kuelimisha, kuendeleza na kunufaisha jamii?

Huu ni mwaka 2015. Kama kupendana bure, tushapendana vya kutosha. Kama kutukanana bila sababu, tushatukanana vya kutosha. Kama kushabikia vitu ambavyo havina msaada wowote kwa sisi na familia zetu, tushashabikia vya kutosha.

Imefika hatua ya kunyanyuana, sio kushushana. Kuelimishana, sio kusemana. Kupeana moyo, sio kukatishana tamaa.

Imefika hatua ya kutegemea mabadiliko, na kupigania mabadiliko.

Nakuomba wewe kaka angu, dada angu, mama angu, baba angu...nakuomba ufanye maamuzi leo, kwamba kesho yako haitakua kama jana yako.

Kwa jina naitwa Wema Sepetu. Na leo hii nimeamua kwamba kesho yangu, haitakua kama jana yangu!

Wewe je? “.-Wema  mwenye followers zaidi ya laki nne mtandaoni ameandika haya na kuungwa mkono na mashabiki wengi na hata wale wanomdisi.

Asante sana Wema, ujumbe umefika.

Kwa jina naitwa Mzee wa Ubuyu  na leo hii nimeamua kesho yangu haitakauwa kama jana yangu.

11.03.2015 -  Tags:  WEMA
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

11 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. UMAANISHE UNACHOSEKISEMA.!!!!

    ReplyDelete
  2. Sasa kama ndio hivyo na ww uache mambo yasio namaana kwa jamii,tunataka uwe mfano mzuri,sio kutwa kurusha mapicha na maneno ya kijinga mitandaoni

    ReplyDelete
  3. tena uwaambie na hao vibwengo wafuasi wako waache kuchafua hali ya hewa mtandaoni kwa maneno yasiyo na hesima. IT BEGINS WITH YOU I mean you Wema Sepetu

    ReplyDelete
  4. Anze kuonesha mfano mzuri wanhine waige na icho kipindi chake cha kipumbavu anatowa hakuna chamana hata kimoja nenda hospital jatembeleye wagonjwa nenda katembeleye waze nenda kwa watoto yatima siyo ubatowa upumbavu mtupu uko club unatukana watu unafundisha nini kwanza jirekebishe kwanza ilo sono unetowa siyo dogo watu wote watakutizama unebadilika vipi

    ReplyDelete
  5. THEY SAY CHARITY STARTS AT HOME IF U KNOW WHATTAM SAYIN'

    ReplyDelete
  6. kamaanisha Wema ndo maana kaandika upo bibi.

    ReplyDelete
    Replies
    1. KAMA KAAMANISHA MBONA ANAMTOLEA MANENO KAJALA???????????

      Delete
  7. nakupendaga sana wema. ..kesho yangu haitakua kama jana yangu

    ReplyDelete
  8. Mjasiri huwa haachi asili yani sijui ni wajinga wangapi leo wataingia kwenye mtego wa kijinga kama huo inaonekana umri umeenda sasa unabadilika tabia bila kujua na unaanza kuomba suluhu kwani huna uwezo wa kujibu mashambulizi kama ilivyokuwa awali sasa unapigwa za uso unaomba suluu ngoja wakutandike kwanza hamu iwaishe

    ReplyDelete
  9. Aaaaaaahhhhh sasa umekuwa. Umri umeenza kukutupa mkono na ndio umeanza kuyajua hayo leo.......mamaeee na bado. Utayajua mengi sana. Wakati ule unashauriwa ulikuwa unaona watu wajinga. Sasa leo hii eti na wewe umekuwa mshauri. Kweli asiyefunzwa na Mama yake hufunzwa na Dunia!!

    ReplyDelete
  10. Na huo ni unafiki mkubwa ambao sijapata kuuona katika maisha pale unaposema kuwa ni wakati wa kunyanyuana na sio kushushana....sio kusemana...na sio kukatishana tamaa. Wakati wewe mwenyewe kila kukicha umekuwa ukimsema Kajala kwa kumtukana na kumdhalilisha. Acha unafiki katika maisha wewe.......Mnafiki mkubwa weweeee.

    ReplyDelete

Top Post Ad