AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA
Akitoa agizo hilo leo mbele ya Waandishi wa Habari, Waziri Wasira amewataja Watendaji hao kuwa ni Bwana Aloyce L. Masanja – Kaimu Mkurugenzi Mkuu; Bibi Tabu Ndatulu – Mkurugenzi wa Mipango na Uwekezaji; na Bwana Filozi John Mayayi – Mkurugenzi wa Fedha na Utawala.
Wassira amesema baada ya Ofisi yake kupata malalamiko kutoka kwa wananchi wa vijiji vya Rufiji pamoja na wawekezaji juu ya Urasimu wa shirika hilo, aliunda timu ya Uchunguzi kutoka wizara ya Kilimo na Hazina kwenda kuchunguza malalamiko hayo.
“Baada ya kuunda tume kutoka hapa Wizarani ikishirkiana na Hazina, walienda kwenye shirika hilo kufanya ukaguzi.Tume ilibaini kwamba mfumo wa pale ulikuwa ni mbovu, wakurugenzi hawa walijifanya wahasibu, wakawa wanakuanya pesa wenyewe na kutembea nazo.Walifanya maksudi tu ili kujiwekea mianya ya kuiba Fedha” Amesema Wassira
Taarifa ya Mheshimiwa Wasira imeanisha kuwa kati ya shilingi 2.748 billion zilizokuwa zimekusanywa kwa ajili uwekezaji, ni shlingi 714.606 milioni tu ndizo zimetumika kihalali wakati kiasi kilichobaki kimetumika bila kuzingatia sheria na kanununi za fedha za umma.
Waziri Wassira amesema kuwa mbali ya kuiba pesa hizo, kamati ilibaini kwamba watendaji hao wametumia zaidi ya Milioni 314 kwenye matumizi yaliyo kinyume cha utaratibu
ikiwemo pesa zilizotengwa kwa ajili maendelea ya miradi ya Shirika hilo ambazo zimetumika ndivyo sivyo.
Vilevile Waziri Wassira amesema hata pesa ambazo wamewakata wafanyakazi kwa ajili ya kupelekwa kwenye mifuko ya Hifadhi ya Jamii zimekuwa zikiliwa na watendaji , tena kwa makusudi pasipo kupelekwa huko.
Aidha,Waziri Wasira amesema baada ya kupata Ripoti ya Tume hiyo ameiagiza Bodi ya shirika la Ludaba kuwafukuza kazi mara moja watendaji hao watatu na nafasi zako kujazwa mara moja huku taratibu na sheria za kuwafikisha mahakamani zikifanyika.
Toa Maoni yako Hapa Chini
Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.
Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA
Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.
NAFASI ZA AJIRA
JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA
GOODLUCK
Duh hongera MH.Wasira, huyo Masanja kaulize bonde la Kilombero ndo wanamjua vizuri Masanja.
ReplyDelete